Uhusika wa Kitoto katika Vibonzo Jongevu

Mbinu ya Kisanaa ya Kuivuta Hadhira ya Watoto

Authors

  • Shadidu Abdallah Chuo Kikuu cha St. John’s cha Tanzania Author

Keywords:

Uhusika, Uhusika wa Kitoto, Vibonzo Jongevu

Abstract

Makala haya yanajadili matumizi ya uhusika wa kitoto katika kazi za Vibonzo Jongevu na uumuhimu wake katika kuivuta hadhira ya watoto. Uchunguzi uliozaa makala haya uliongozwa na malengo makuu matatu. Mosi, kuchunguza mbinu za kitoto zinazotumika katika kazi za Vibonzo Jongevu. Pili, sababu za kutumika kwa mbinu hizo. Na tatu umuhimu wa mbinu hizo kwa hadhira ya watoto. Kazi teule zilizotumika ni za Ubongo Kids, The Adventures of Abney and Teal na Dora the Explorer. Uteuzi wa kazi hizi ulisukumwa na ukweli kuwa watunzi wake hutumia mbinu nyingi zenye mwegamo wa kitoto na hivyo kuivuta sana hadhira ya watoto. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Mwitikio wa Msikilizaji ambapo mtafiti alitumia baadhi ya misingi ya nadharia katika kuchambua na kujadili data zake. Kwa jumla, imebainika kuwa watunzi wa Vibonzo Jongevu hutumia mbinu mbalimbali za kitoto katika utengenezaji wa kazi zao. Mbinu hizi ni pamoja na matumizi ya wahusika watoto, rangi za kuvutia, matendo ya kitoto, motifu za kitoto na uchanganyaji wa wahusika. Ni wazi kuwa, matumizi ya mbinu hizi yamelenga kuongeza idadi ya hadhira na mvuto wa sanaa kwa hadhira ya watoto.

Downloads

Published

01-09-2020

Issue

Section

Articles