Motifu ya Utaifa katika Bunilizi za Kihistoria za Watoto za Mugyabuso Mlinzi Mulokozi

Ubainifu Wake, Sababu na Umuhimu wa Motifu Hiyo

Authors

  • L.H. Bakize Chuo Kikuu cha Zimbabwe Author

Keywords:

Motifu, Motifu ya Utaifa, Bunilizi za Kihistoria za Watoto, Nadharia ya Uoniafrika

Abstract

Wachambuzi mbalimbali wa fasihi wamekuwa wakisisitiza kwamba urudiaji unaojitokeza katika kazi mbalimbali za mwandishi mmoja husukumwa na nia ya mwandishi husika kutaka kusisitiza jambo fulani (taz. Okpewho, 1992; Ntarangwi, 2004;Senkoro, 2011). Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Kimbi (2016) katika kazi tatu za Mulokozi, unaonesha kwamba, tofauti na ilivyokuwa inachukuliwa hapo awali, urudiaji wa dhamira katika kazi za fasihi una dhima nyingi zaidi ya ile ya kusisitiza jambo. Utafiti wa Kimbi (2016) unabainisha kwamba Mulokozi alirudia dhamira ya uzalendo katika vitabu vyake vitatu, yaani Ngoma ya Mianzi (1991), Ngome ya Mianzi (1991) na Moto wa Mianzi (1996) kwa nia ya kuweka msisitizo, kukamilisha hadithi au kisa kilichopaswa kukamilika katika vitabu vyote vitatu, kuonyesha falsafa ya mwandishi, n.k. Bila kurudufu matokeo ya utafiti huo wa Kimbi, makala haya yanakusudia kuchambua motifu ya utaifa katika kazi nne za Mulokozi, yaani Ngoma ya Mianzi (1991), Ngome ya Mianzi (1991) Moto wa Mianzi (1996) na Utenzi wa Nyakiiru Kibi (1997). Kwanza makala inavichambua vitabu husika kwa kuangalia namna motifu ya utaifa inavyojitokeza. Pili, makala inatoa ufafanuzi wa kwa nini mwandishi aliamua kutumia motifu hiyo katika kazi zake. Mbali na uchambuzi wa vitabu teule, makala yametumia pia data za uwandani zilizopatikana kutoka katika mahojiano maalumu aliyoyafanya mwandishi wa makala na mwandishi wa vitabu teule. Makala yanaongozwa na mwega wa Nadharia ya Uoniafrika, ambayo hudai kwamba kazi za kifasihi za Kiafrika zinaweza kueleweka kwa usahihi zaidi kwa kujikita katika mazingira ya kijadi na historia ya jamii husika za Kiafrika. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba kazi teule zilizochambuliwa zina maudhui muhimu yenye mchango mkubwa katika ujenzi wa dhana ya utaifa kwa watoto. Makala yanachambua motifu ya utaifa kwa kina na kisha kuonyesha thamani ya kazi teule katika kuwaandaa watoto wa Kitanzania kuipenda nchi yao na kuitumikia kwa moyo wa umoja.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles