Uchanganuzi wa Toni katika Ushairi wa Kithaka wa Mberia

Authors

  • Samson Ontiri Ongarora Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • James Nyachae Michira Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Rayya Timammy Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Kineene wa Mutiso Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Toni, Ushairi, Uchanganuzi, Uhakiki wa Fasihi, Kinaya, Tashtiti, Huzuni

Abstract

Suala la mtazamo na hisia ni muhimu katika uhakiki wa fasihi hususan ushairi. Uchanganuzi wa mashairi hauna budi kutambua kuwa mshairi hutumia maneno na miundo ya sentensi ili kuwasilisha mtazamo au mawazo fulani. Kwa hivyo, ili kufahamu mawazo yanayowasilishwa na mshairi, ni muhimu kuchunguza toni ya mashairi yake. Baadhi ya maswali yanayodokeza toni ya mshairi ni haya yafuatayo. Je, mshairi anasema jambo fulani kutokana na matazaomo gani? Je, ikiwa shairi hilo lingesomwa hadharani, sauti yake ingesikika vipi? Je, mshairi “anaongea” kwa hasira, ucheshi au uchungu? Je, anatumia maneno au msamiati unaoelekeza? Tungo nyingi za kishairi hutegemea mbinu ambazo huziwezesha kuwasilisha ujumbe wake kwa athari kubwa. Huu hasa ndio msingi wa kuzungumzia hisia katika shairi. Suala la hisia huweza kufungamanishwa kwa kiasi kikubwa na dhana ya toni. Sauti inayosikika katika utungo wa kishairi huwa na mchango mkubwa katika uwasilishaji wa maana katika mashairi. Matarajio ya msomaji au msikilizaji ni kuwa utungo unaohusu jambo la huzuni, ucheshi, kinaya au uchungu utakuwa na uteuzi wa maneno, msamiati na sentensi zinazoweza kuibua athari iliyokusudiwa na mwandishi au mzungumzaji. Katika makala haya,  tunachanganua kipengele cha toni kwa undani kama kinavyojitokeza katika baadhi ya mashairi ya Kithaka wa Mberia katika diwani zaMchezo wa Karata(1997), Bara Jingine (2001), Redio na Mwezi (2005), Msimu wa Tisa (2007) na Rangi ya Anga (2014). Tunachanganua namna toni za uchungu, furaha, huzuni, tashtiti na kinaya zinadhihirika na ufaafu wake katika ujumbe anaouwasilisha mshairi.

Downloads

Published

01-09-2020

Issue

Section

Articles