Kiswahili na Sera ya Elimu katika Shule za Sekondari Nchini Kenya

Authors

  • Dunstan Kwova Egessa Chuo cha Ualimu cha Migori Author
  • Isaac Ipara Odeo Chuo Kikuu cha Kibabii Author

Keywords:

Sera ya elimu, Kiswahili, Utekelezaji, Kenya

Abstract

Makala haya yanachunguza matatizo yanayowakumba walimu katika utekelezaji wa silabasi ya sasa ya Kiswahili. Utafiti ulifanywa katika Kaunti ya Kakamega, Mkoa wa Magharibi nchini Kenya. Sampuli ya watafitiwa iliteuliwa kwa kutumia mbinu za utabakishaji, uwiano na njia nasibu sahili. Walimu 70 na walimu wakuu 43 walishiriki katika utafiti. Afisa wa Usanifu wa Viwango vya Elimu mmoja na Mkuza mitalaa mmoja katika Taasisi ya Elimu Kenya walishiriki kama watafitiwa maalumu. Nyenzo za ukusanyaji data ambazo zilitumiwa ni hojaji, mwongozo wa masaili na mwongozo wa uchunzaji. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uwezeshaji ya Carl Rodgers. Utafiti uligundua kwamba utekelezaji wa silabasi ya sasa ya Kiswahili unakumbwa na matatizo mbalimbali. Sababu za hali hii ni kuwa, walimu hawakuandaliwa mapema kabla ya kuanzishwa kwa silabasi hii na wengi katika vyuo hawakujifunza baadhi ya mada katika silabasi ya sasa ya Kiswahili. Walimu, vile vile, hawaandaliwi mafunzo nyanjani na walimu hawajiandai vyema kitaaluma. Ili walimu waweze kufaulisha utekelezaji wa silabasi, utafiti umependekeza kuwa, Taasisi ya Elimu ya Kenya iandae semina kadhaa kwa walimu Kauntini ili masuala nyeti katika silabasi yafafanuliwe. Wizara ya Elimu yafaa itenge fedha za kufadhili mafunzo kwa walimu kwa Kiswahili nyanjani pamoja na usimamizi. Aidha, vyuo vinavyoandaa walimu wa shule za upili vitilie maanani mada ambazo zinajumuishwa katika mitalaa ya shule za upili. Mwisho walimu wazingatie maadili ya kazi yao.

Downloads

Published

30-04-2017

Issue

Section

Articles