Matumizi ya Vielelezo vya Kihisabati katika Fafanuzi za Fahiwa Mbalimbali
Keywords:
Fahiwa, hisabati, vielelezo, isimuAbstract
Isimu ni taaluma ya sayansi ya lugha ya binadamu. Usayansi huu unaorejelewa katika uchanganuzi wa lugha huzingatia sifa anuwai hasa uwazi, utaratibu na urazini au kutoa uamuzi kulingana na data inayorejelewa. Ingawa masuala ya kiisimu hushughulikiwa katika makala mbalimbali kwa kutumia vielelezo maalum vya kiisimu, inabainika vilevile kuwa kuna uwezekano wa kutumia vielelezo teule vya kihisabati katika fafanuzi za dhana anuwai katika isimu. Ingawa vielelezo hivi vinadhihirika katika hisabati, tafiti nyingi zinaonyesha vilevile kuwa vinaweza kutumiwa kikamilifu katika tawi la isimu linalojulikana kama isimu kihisabati. Hivyo basi, makala haya yanazungumzia jinsi tunavyoweza kutumia kikamilifu vielelezo vya kihisabati katika fafanuzi za fahiwa mbalimbali katika Kiswahili. Makala yanadhamiriwa kutoa mchango mkubwa katika mafunzo ya semantiki kileksika pamoja na taaluma ya isimu kihisabati.