Changamoto za Kuueleza Msamiati wa Samaki

Mtazamo wa Kiuhusiano

Authors

  • John Habwe Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Rayya Timammy Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • Amir Swaleh Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Msamiati wa Samaki, Changamoto, Kiuhusiano

Abstract

Makala haya yanachunguza maelezo ya majina ya samaki katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Kwa kutumia nadharia ya kiuhusiano imebainika kuwa kunatumika vichocheo au mikakati tofauti tofauti ili kumweleza samaki. Hata hivyo, licha ya vijenzi hivi kutumika bado kuna changamoto nyingi kama vile maelezo fulani kukosa uangavu kwa kuwa ni mapana zaidi au kutochangia kikamilifu katika kumweleza samaki kwa kuwa ni maelezo finyu, kutotumia vichocheo vya kutosha au kichocheo kimoja ambapo vichocheo vingi vingefaa zaidi. Aidha, imebainika kuwa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) imetumia vichocheo vya tabia, chakula, rangi, umbo, vumba na hata picha ili kuwaeleza aina ya samaki ili wasomaji waweze kuwatambua na kuwaeleza. Licha ya vichocheo hivi, ni wazi kuwa KKS bado inakabiliwa na changamoto ya kuwaeleza samaki kwa uwazi, uangavu na kwa kukinaisha.

Downloads

Published

30-04-2017

Issue

Section

Articles