Ubainikaji wa Mahusiano na Mamlaka kupitia Usemi kwenye Nyumba za Watawa za Malezi

Authors

  • Teresia W. Waweru Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • John Habwe Chuo Kikuu cha Nairobi Author
  • P. I. Iribemwangi Chuo Kikuu cha Nairobi Author

Keywords:

Namna, Mahusiano, Vitenzi Leksika, Walelewa, Walezi

Abstract

Utafiti huu unahusu kujieleza na ubainikaji wa mahusiano na mamlaka yanayowezeshwa kupitia matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye nyumba za watawa za malezi katika kanisa Katoliki nchini Kenya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Sarufi amilifu msonge ya Michael Halliday (1985). Data ya uchunguzi ya utafiti huu ilikusanywa kutoka nyanjani katika nyumba za malezi mjini Mombasa ambapo lugha ya Kiswahili hutumika kwa kiasi kikubwa na ni mojawapo ya lugha kuu za mawasiliano. Matini zilizoangaziwa zilikuwa katika kiwango cha kishazi na sentensi. Maswali matatu yaliyopaniwa kujibiwa na makala haya ni kwamba je, lugha hutumiwa vipi kati ya walezi na walelewa wakati wa kujieleza. Pili, je mamlaka hubainikaji vipi kwenye mawasiliano katika nyumba za watawa za malezi? Tatu je, mamlaka na mahusiano hudhihirika vipi katika matumizi ya lugha iliyo rasmi na isiyo rasmi katika nyumba za watawa za malezi? Matokeo ya utafiti yanatanaonyesha kuwa kujieleza na ubainikaji wa mahusiano na mamlaka yasiyo wazi kati ya walezi na walelewa hudhihirika katika usemi katika nyumba za watawa kupitia matumizi ya lugha ya Kiswahili.

Downloads

Published

30-09-2023

Issue

Section

Articles