Kanuni za Kifonolojia za Uingizaji wa Vinyambuo Vitenzi katika Kamusi

Mifano kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2013)

Authors

  • Fatuma Abdallah Baraza la Kiswahili la Taifa, Tanzania Author

Keywords:

Fonolojia, Kanuni, Vitenzi, Kamusi

Abstract

Utungaji kamusi ni kazi ya kisayansi ambayo mbali na mambo mengine inahusisha matawi mbalimbali ya isimu. Katika kusisitiza suala hili, Mdee (2010) anaeleza kwamba mwanaleksikografia anawajibika kufahamu japo kwa uchache maarifa ya nyanja za isimu ili yamsaidie katika kueleza leksimu anazoziteua na kuziingiza katika kamusi. Maelezo haya yanadhihirisha kwamba ni muhimu maarifa ya nyanja mbalimbali za isimu yakazingatiwa wakati wa kuingiza vidahizo na taarifa katika kamusi ikiwamo vinyambuo vitenzi. Makala haya yanalenga kufafanua kanuni za kifonolojia zilizozingatiwa wakati wa kuingiza vinyambuo vitenzi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la tatu (kuanzia sasa KKS 3). Pia makala haya yanaeleza athari za kutokufuata kanuni hizo na itatoa mapendekezo ya nini kifanyike ili uingizaji wa vinyambuo vitenzi uwe wa ufanisi zaidi katika kamusi mbalimbali za Kiswahili ikiwa ni pamoja na Kiswahili Sanifu.  

Downloads

Published

30-04-2019

Issue

Section

Articles