Mwingiliano wa Kanuni za Kimofosintaksia wa Ngeli Nomino za Luganda katika Matumizi ya Kiswahili Sanifu

Authors

  • Martin Mulei Chuo Kikuu cha Kabale Author
  • Beverlyne Asiko Ambuyo Chuo Kikuu cha Maseno Author
  • Debora Nanyama Amukowa Chuo Kikuu cha Maseno Author

Keywords:

Mwingiliano, Kanuni, Mofosintaksia, Ngeli, Nomino, Kiswahili

Abstract

Makala haya yanalenga kuweka wazi mwingiliano wa kanuni za kimofosintaksia wa ngeli za Luganda katika matumizi ya Kiswahili sanifu. Utafiti huu unatokana na tafiti za awali zilizobainisha kuwa Kiswahili kinachozungumzwa na kuandikwa na Wanauganda ni kile kinachokiuka kanuni na miundo ya kisarufi ya Kiswahili sanifu. Aidha, Luganda na Kiswahili sanifu ni lugha za Kibantu ambazo hutumia mfumo mmoja wa uainishaji wa ngeli, na uwiano na tofauti za kanuni za matumizi ya ngeli kimofosintaksia huweza kusababisha mwingiliano baina ya lugha mbili tofauti. Data ya makala haya ilitokana na uchanganuzi wa mazungumzo na maandishi ya wanafunzi 117 wa shule za upili 15 teule wilayani Kampala, Uganda ambao L1 ni Luganda. Utafiti huu uliongozwa na mihimili ya usarufi bia na upatanifu wa nadharia ya Umilikifu na ufungamanisho (Chomsky, 1981) ambayo hudhihirisha hali ya vipashio fulani vya kisarufi kutawala na kumiliki vipashio vingine katika tungo. Kupitia kwa mijadala, usaili, uandishi na usimulizi wa insha na mijarabu ya kisarufi, matokeo yalidhihirisha wanafunzi kuhamisha, kuchanganya, kubadilisha, kuongeza na kujumlisha kanuni za kimofosintaksia za matumizi ya ngeli katika maandishi na mazungumzo ya Kiswahili sanifu. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuwaongoza walimu na wanafunzi wa Kiswahili kutambua mchango wa lugha asili katika matumizi, ujifunzaji na ufundishaji wa L2, kutofautisha kanuni za Luganda na Kiswahili sanifu na athari zake katika Kiswahili sanifu na uimarishaji wa matumzi ya Kiswahili sanifu.

Downloads

Published

30-09-2021

Issue

Section

Articles