Ubadilishaji Msimbo kama Mbinu ya Upole Chana katika Vipindi vya 'Sobetab Kapchi' kwenye Idhaa ya KASS FM

Authors

  • Muge Tecla Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Upole Chanya, Upole Hasi, Kuokoa Uso, Sobetab Kapchi, KASS FM

Abstract

Makala haya yanahusu nafasi ya ubadilishaji msimbo kama mbinu ya upolekatika vipindi vya Sobetab Kapchi (SK) katika idhaa ya KASS FM. Utafiti uliongozwa na maswali mawili: je, wahusika katika vipindi vya SK wanachopeka maneno ya Kiswahili kwenye mazungumzo yao? Je, huku kubadilisha msimbo kunatokea katika hali zipi? Aidha, utafiti ulielekezwa na Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1987), hasa kipengele cha kuokoa uso. Vipindi vinne vya mazungumzo ya SK vilinaswa. Data zilizohusiana na upole kutoka kwa vipindi husika zilinakiliwa na kuchanganuliwa. Baadhi ya data zilinukuliwa moja kwa moja na zingine zilifupishwa kutegemea urefu wa data. Ilibainika kuwa, wasemaji wa Kinandi katika mazungumzo ya SK huchopeka maneno ya Kiswahili kwenye mazungumzo yao. Aidha, UM hutokea wakati wasemaji wanafikiria kuwa neno la Kinandi linaweza kutishia nyuso za wahusika wa mazungumzo.

Downloads

Published

30-09-2018

Issue

Section

Articles