Kufanana na Kutofautiana kwa Konsonanti katika Msamiati wa Kipemba na Kingazija

Authors

  • Sauda Uba Juma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Konsonati, Msamiati, Sauti, Lugha-Mame

Abstract

Makala haya yanahusu ulinganishaji wa mfumo wa saui za konsonati baina ya Kipemba na Kingazija kwa lengo la kubaini mfanano na tofauti zilizopo baina yake. Data za makala haya zilikusanywa uwandani katika mazingira chasili ya wazawa wa lugha kupitia mbinu za hojaji na mahojiano. Matokeo tuliyoyapata kutoka kwa watoataarifa yameonesha kuwapo kwa mfanano na tofauti za mfumo wa sauti za konsonanti katika Kipemba na Kingazija. Hata hivyo, pamoja na tofauti za hapa na pale, tunathubutu kusema kuwa, Kipemba na Kingazija ni lugha ambazo zinatokana na lugha-mame moja, kwani tofauti hizo ndogondogo zilizojitokeza, imebainika kuwa zimetokana na utengano wake wa muda mrefu pamoja na umbali wa kijiografia uliopo miongoni mwake.

Downloads

Published

30-09-2020

Issue

Section

Articles