Lugha, Fasihi na Ukabila

Mwelekeo wa 'Nasikia Sauti ya Mama'

Authors

  • Deborah Nanyama Amukowa Chuo Kikuu cha Maseno Author

Keywords:

Fasihi, Lugha, Ukabila, Ujima

Abstract

Ukabila ni dhana ambayo inajidiliwa katika vyombo vya habari na wanasiasa na hata wananchi wa kawaida wameipa dhana hii nafasi katika mazungumzo yao ya kila siku. Hivyo basi, ukabila umekita mizizi katika harakati za maisha ya watu. Inaaminika kuwa dhana hii ilizuliwa na watu wachache wenye nia ya kukidhi matakwa yao kisiasa ili kujinufaisha na mfumo wa maisha ambao utawafanya watu wengine katika jamii kujiona wametengwa na kubaguliwa. Ukabila umesababishwa na ubinafsi wa watu wanaojiweka mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu ya maendeleo katika jamii ambayo ina watu wenye mtazamo, itikadi, dini, lugha na tamaduni tofauti. Tofauti hizi husababisha jamii moja kujitenga na nyingine na kuibua matabaka ya watu ambao kila mmoja anajiona bora kuliko mwenzake. Makala haya basi yatajadili suala la ukabila kwa kurejelea riwaya, tawasifu/bayografia ya Nasikia Sauti ya Mama mintaarafu lugha ya Kiswahili iliyotumiwa katika utunzi wake.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles