Mabadiliko ya Kimofofonemiki katika Msamiati Mkopo wa Kikipsigis

Authors

  • Naomi J. Cherono Chuo Kikuu cha Moi Author
  • John G. Munyua Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Nathan O. Ogechi Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Msamiati Mkopo, Utohozi, Mabadiliko ya Kimofofonemiki

Abstract

Kila lugha ni mfumo huru unaojitosheleza kisarufi. Ingawa hivyo, wasemaji wa lugha tofauti wanapotagusana kimawasiliano, lugha zao huweza kuathiriana kisarufi, na athari mojawapo huwa ni ukopaji wa msamiati. Ni kutokana na hali hii ambapo utafiti huu ulichunguza kanuni zinazofuatwa katika uingizwaji wa msamiati mkopo wa Kiswahili na Kiingereza katika Kikipsigis. Makala haya yalichunguza mabadiliko ya kimofofonemiki yanayotokea katika msamiati mkopo unapoingizwa katika mfumo wa Kikipsigis. Vilevile, sababu za ukopaji zilibainishwa. Data ya utafiti iliteuliwa kimakusudi. Utafiti ulitambua kuwa Kikipsigis hufupisha irabu ndefu katika msamiati mkopo. Vilevile, irabu unganifu husahilishwa ili zikubalike katika Kikipsigis. Kimsingi tulitambua kuwa Kikipsigis hutohoa irabu ngeni kwa kutumia irabu asili zinazokaribiana kimatamshi. Ilibainika pia kwamba Kikipsigis hakiruhusu mfuatano wa konsonanti mwanzoni mwa neno. Kwa hivyo, Kikipsigis hutohoa msamiati wa aina hii kwa kuchopeka irabu. Katika kuchunguza vichocheo vya ukopaji, makala haya yalibainisha kwamba Kikipsigis hukopa msamiati ili kurejelea dhana ngeni isiyokuwepo katika utamaduni wake. Hata hivyo, uchanganuzi ulionyesha kuwa Kikipsigis wakati mwingine hukopa msamiati hata kama kina msamiati asilia kwa sababu ya ubadilishaji msimbo, msamiati mkopo ni sahili na rahisi kutamkwa ukilinganishwa na kisawe chake cha Kikipsigis.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles