Majina Fiche ya Asili Wanayopewa Watu na Uchanuzi wake wa maana katika Lugha na Semi za Kiswahili
Keywords:
Majina Fiche, Lugha, Semi, Kiswahili, Asili, WatuAbstract
Azma ya makala haya ni kuonesha jinsi majina majina ya asili yenye maanafiche wanayopewa watu yanavyochanuza maana tofauti katika lugha ya Kiswahili. Watu wa jamii mbalimbali wana desturi ya kuwapa watoto wao majina yenye maana iliyojificha kwa malengo maalumu. Malengo hayo yanaweza kutokana na mazingira au vigezo mbalimbali vinavyosababisha watu wa jamii zingine kuwapa watoto wao majina ya namna hiyo. Pamoja na ukweli huo, bado baadhi ya watu hawajaelewa sawasawa maana ya majina hayo katika Kiswahili. Hivyo basi katika makala haya tumejikita zaidi na kuangazia majina hayo yanatoa maana gani katika lugha ya Kiswahili na jinsi maana hizo zinavyoakisi semi mbalimbali za Kiswahili. Data za makala haya zilikusanywa uwandani kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili, mahojiano, udusuru wa nyaraka mbalimbali pamoja na kamusi ili kuapata maana ya majina hayo. Aidha, uchanganuzi wa data na uwasilishaji wake, ulitumia njia ya kitaamuli na wakati mwingine data zilichambuliwa kitakwimu. Zaidi ya hayo nadharia ya semiotiki ilitumika kuogoza uchanganuzi wa data za makala haya.