Uasilishaji wa Maneno ya Kigeni katika Lugha za Kiafrika

Mfano wa Kitharaka

Authors

  • Mwenda Mukuthuria Chuo Kikuu cha Maasai Mara Author
  • Kimathi Mwembu Chuo Kikuu cha Chuka Author
  • Enock Matundura Chuo Kikuu cha Chuka Author

Keywords:

Uasilishaji, Fonolojia, Kitharaka, Maneno ya Kigeni, Lugha za Kiafrika

Abstract

Kila lugha hukopa maneno ya kigeni na kisha kuyaasilisha ili yaafiki mfumo wa kifonolojia wa lugha pokezi. Kitharaka ni lugha iliyokopa maneno na kuyaasilisha kwa mujibu wa mfumo wa fonolojia yake. Makala haya yanaweka wazi mchango wa michakato ya kifonolojia katika kufanikisha uasilishaji wa maneno ya kigeni katika Kitharaka. Kitharaka ni lahaja ya lugha ya Kimeru inayozungumzwa nchini Kenya. Uasilishaji wa maneno ya kigeni kutoka lugha mbili changishi (ambazo ni Kiswahili na Kiingereza) hadi Kitharaka umeangaziwa. Jumla ya michakato minane ya kifonolojia imeshughulikiwa kama vile uchopekaji wa sauti, kuimarika kwa fonimu, kudhoofika kwa fonimu, ukaakaishaji, ung’ong’oishaji, usilimisho, usilabishwaji na uwiano wa irabu. Hatimaye, makala haya yamependekeza uchunguzi zaidi ufanywe ili kuweka wazi jinsi michakato ya kifonolojia katika Kitharaka inavyokamilishana. Vilevile, makala haya yamependekeza uasilishaji wa maneno ya kigeni katika lugha nyingine za Kiafrika uchunguzwe ili kubainisha jinsi lugha hizi zinavyokamilishana na kufaana kukabiliana na changamoto za mawasiliano katika kipindi hiki cha utandawazi.

Downloads

Published

30-04-2017

Issue

Section

Articles