Makosa ya Kimatamshi Yanayofanywa na Wazungumzaji wa Kiswahili wa Mkoa wa Mara nchini Tanzania

Authors

  • Nyanjura Sabato Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Author

Keywords:

Matamshi, Kiswahili, Tanzania, Lugha yao ya Pili, Uchopekaji, Jamiilugha

Abstract

Makala haya yamechunguza makosa ya kimatamshi yanayofanywa na wazungumzaji wa Kiswahili wanaoishi katika mkoa wa Mara nchini Tanzania. Suala hili linasababishwa na changamoto ambazo wanakumbana nazo wazungumzaji katika harakati za kujifunza Kiswahili ambayo ni lugha yao ya pili (L2). Hata hivyo, katika harakati za kuzungumza Kiswahili wazungumzaji hao wamejikuta wakikabiliwa na makosa ya udondoshaji wa baadhi ya sauti, uchopekaji wa sauti na ubadilishaji wa sauti. Dane (1990) anaeleza kuwa mwingiliano wa lugha unahatarisha lugha kwani husababisha lugha moja kubadilika, kuchanganyika na lugha nyingine hata kufa. Aidha, imebainika kuwa makosa hayo husababishwa na sababu kadhaa ambazo zimewafanya wazungumzaji hao kutumia kimakosa kanuni za lugha ya Kiswahili. Mbinu za mahojiano na dodoso zilitumika kupata data za utafiti huu. Uchunguzi huu umeongozwa na Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia iliyoasisiwa na Chomsky na Morris (1968). Nadharia hii ilitusaidia kubaini makosa ya udondoshaji wa sauti, uchopekaji wa sauti, ubadilishaji wa sauti na sababu za kuwapo kwa makosa hayo. Khansir (2012) anabainisha kuwa kila lugha ina muundo wake wa sauti na mpangilio wa maneno. Uhamishaji wa muundo wa lugha ya kwanza katika lugha ya pili hudhihirika kama makosa. Kutokana na mwingiliano huo wanajamiilugha waliopo katika mkoa wa Mara wamekuwa wakizungumza lugha ya Kiswahili huku wakiwa wanakabiliwa na baadhi ya makosa.

References

Abawi, L. (2013). School Meaning Systems: The Symbiotic Nature of Culture and ‘Language-in-Use.’ Improving Schools, 16(2), 89–106. Retrieved from

http://journals.sagepub.com/doi/ 10.1177/1365480213492407

Chimerah, R. (1998). Kiswahili Past Present and Future Horizons. Nairobi University Press.

Chomsky, N., & Morris, H. (1968). The Sound Pattern of English (ERIC Ed.). Institute of Education Sciences FAQ.

Dane, F. C. (1990). Research Methods. Thomason Books Publishing Co.

Darus. (2005). Athari za Lugha katika Lugha ya Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.

Gas, S. (1979). Language Transfer and Universal Grammatical Relations. Language Learning, 29(2), 327–344. Retrieved from https://onlinelibrary.wiley.com/doi/10.1111/j.1467-1770.1979.tb01073.x

Khansir, A. A. (2012). Error Analysis and Second Language Acquisition. Theory and Practice in Language Studies, 2(5), 1027–1032.

Kihore, Y. M., Massamba, D. P. B., & Msanjila, Y. P. (2003). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA): Sekondari na Vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo kukuu cha Dar es Salaam.

Kindole, E. (2020). Matumizi ya Alama za Kifonetiki za Kimataifa katika Uwasilishaji wa Taarifa za Kimatamshi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu Toleo la 3. Kioo cha Lugha: Journal of Language, Technology & Entrepreneurship in Africa, 17(1).

Kipacha, A. (2016). Utangulizi wa Lugha na Isimu OSW 101, (August).

Kisakwah, B. A. (2014). Uchanganuzi Makosa na Muundo Sentensi: Ulinganisho wa Sentensi Sahili za Kiswahili Sanifu na za Kisuba. University of Nairobi.

Kishe, A. (2016). Kuingiliana kwa Lugha ya Kiswahili na Kiingereza: Uswahilishaji wa Maneno ya Kiingereza. Huria: Journal of the Open University of Tanzania, 21(1), 91–105.

Massamba, D. P. B. (2006). Kiswahili cha Musoma: Mwanzo wa lahaja Nyingine. Kiswahili. Serengeti Publisher.

Matinde, R. S. (2021). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na vyuo Vikuu. Serengeti Educational Publishers Limited.

Mbaabu, I. (1985). New Horizons in Kiswahili: A Synthesis in Developments, Research, and Literature. Kenya Literature Bureau.

Mgullu, R. S. (1999). Mtalaa wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers.

Mochiwa, Z. S. M. (1979). The Impact of Kiswahili Language on Ethnic Languages: A Case Study from Handeni District. University of Dar es Salaam.

Msigwa, A. B. G. (2020). Kioo cha Lugha, 18, 22-35.

Ndekiro, R. (2021). Sababu za Matumizi ya Lugha Tandawazi katika Mtandao wa Facebook na Athari zake katika Kiswahili Sanifu. Mulika Journal, 39(16).

Ngugi, J. K. (2007). Uchunguzi wa Athari za Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi Wakikuyu: Mfano ktutoka katika Tarafa ya Bahati, Nakuru. Chuo Kikuu cha Egerton.

Nyagah, S. K. (2016). Uchanganuzi wa Makosa ya Kifonolojia na Kimofolojia Yanayojitokeza katika Kazi Andishi za Wanafunzi wa Shule za Upili Tigani Jimboni Meru. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili, Nairobi: Chuo Kikuu cha Nairobi.

Ontieri, J. O. (2010). Uchunguzi wa Makosa katika Insha za Wanafunzi wa Shule za Upili.Mfano wa Wilaya ya Nakuru. Chuo Kikuu cha Egerton. Tigania Jimbo la Meru. Tasnifu ya Shahada ya Uzamili. Nairobi: Chuo Kikuu cha Nairobi.

Richards, J. (1974). Analysis, Perspective on Second Language Acquisition in J. C. A. Mon Contractive Aproach to Error Analysis. Africa Education Review, 2, 172–188.

Richards, J. (1971). Error Analysis and Second Language Strategies. Language Sciences.

Downloads

Published

30-09-2024

Issue

Section

Articles

How to Cite

Makosa ya Kimatamshi Yanayofanywa na Wazungumzaji wa Kiswahili wa Mkoa wa Mara nchini Tanzania. (2024). Mwanga Wa Lugha, 9(2), 67-75. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/533