Mabadiliko ya Kifonolojia ya Istilahi za Kiingereza katika Kiswahili
Uchunguzi Kifani kutoka Covid 19
Keywords:
'COVID 19', Huhisha, Fukiza, 'Lockdown', 'Corona', 'Mask & Quarantine'Abstract
Miongoni mwa mambo yanayozifanya lugha kukopa na kutohoa istilahi ni mlipuko wa magonjwa. Gonjwa la COVID 19 limekuwa sababu ya lugha ya Kiswahili ama kukopa, kutohoa au kuhuisha istilahi za Kiingereza. Makala haya yanachunguza mabadiliko ya kifonolojia ya istilahi za Kiingereza katika Kiswahili kwa kujikita katika istilahi zinazohusiana na COVID 19. Katika kuchunguza mabadiliko ya kifonolojia ya utohozi wa istilahi hizo tumeongozwa na nadharia ya NFZ (Nadharia ya Fonolojia Zalishi) iliyoasisiwa na Noam Chomsky na Morris Halle (1968). Nadharia hii ni muafaka katika makala haya kwani inatoa mwongozo katika kuchunguza na kuchanganua mabadiliko ya sauti yanayojitokeza baada ya istilahi kutoholewa kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa. Makala haya yanashughulikia mojawapo ya matokeo ya utohozi unaohusisha lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Ili kufikia malengo ya makala yetu, zimetumika mbinu za hojaji na uchambuzi wa matini. Mbinu ya hojaji hurahisisha ukusanyaji wa data kutoka kwa watafitiwa wengi kwa muda mfupi (Mugenda na Mugenda 2003). Mbinu ya kuchambua matini imejumuisha usomaji wa nyaraka za kitaaluma kwa minajili ya kupata data ya makala yetu.