Utambuzi, Hisia na Mabadiliko ya Kisemantiki katika Leksia za Kiswahili

Authors

  • Tirus Mutwiri Gichuru Chuo Kikuu Cha Kenyatta Author
  • Kitula King’ei Chuo Kikuu Cha Kenyatta Author
  • Ireri Mbaabu Chuo Kikuu Cha Kenyatta Author

Keywords:

Utambuzi, Hisia, Mabadiliko, Leksia, Semantiki Tambuzi

Abstract

Makala haya yamejadili nafasi ya utambuzi na hisia katika mabadiliko kwenye kisemantiki ya leksia za Kiswahili. Makala yanaonyesha namna maarifa katika utambuzi hujenga msingi na kuongoza mbinu na taratibu mbalimbali za mabadiliko ya kisemantiki na hatimaye kuchangia katika mabadiliko ya maana. Mifano mahususi ya leksia kutoka Kiswahili cha kabla ya Karne ya Ishirini na cha Karne ya Ishirini na Moja imelinganishwa ili kudhihirisha mabadiliko husika. Asili ya data ni matini teule za kabla ya Karne ya Ishirini, matini za kilekskografia za Karne ya Ishirini na Moja na kutoka kwa wazungumzaji wa pwani ya Kenya wenye elimu-asilia. Nadharia ya Semantiki Tambuzi imezingatiwa. Imebainika kuwa tajriba na maarifa yaliyofichamwa kwenye utambuzi huwa nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya maana za leksia. Makala haya pia yamedhihirisha mchango na ufaafu wa vigezo vya kiutambuzi vya nadharia ya Semantiki Tambuzi katika kuelezea mabadiliko ya lugha.

Downloads

Published

30-09-2019

Issue

Section

Articles