Utambuzi, Hisia na Mabadiliko ya Kisemantiki ya Leksia za Kiswahili

Authors

  • Tirus Mutwiri Gichuru Chuo Kikuu cha Kenyatta Author

Keywords:

Utambuzi, Hisia, Mabadiliko, Leksia, Semantiki Tambuzi, Taswira, Sitiari, Maarifa

Abstract

Makala haya yamejadili nafasi ya utambuzi na hisia katika mabadiliko ya kisemantiki ya leksia za Kiswahili. Makala yanaonyesha namna maarifa katika utambuzi hujenga msingi na kuongoza mbinu na taratibu mbalimbali za mabadiliko ya kisemantiki na hatimaye kuchangia katika mabadiliko ya maana. Mifano mahususi ya leksia kutoka Kiswahili cha kabla ya Karne ya Ishirini na cha Karne ya Ishirini na Moja imelinganishwa kudhihirisha mabadiliko husika. Asili ya data ni matini teule za kabla ya Karne ya Ishirini, matini za kilekskografia za Karne ya Ishirini na Moja na kutoka kwa wazungumzaji wa pwani ya Kenya wenye elimu-asilia. Nadharia ya Semantiki Tambuzi imezingatiwa. Imebainisha kuwa tajriba na maarifa yaliyofichamwa kwenye utambuzi huwa nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya maana za leksia. Imegunduliwa kuwa kila kuchao utambuzi huzidi kupanuka kiupeo, kufinyika na kugeuka pindi jamii nzima inavyobadilika kutokana na maendeleo ya sayansi, teknolojia, uchumi, jamii na siasa. Kadhalika fasili tofauti za dhana moja, usisitizo na kuipa dhana kipaumbele ni maswala ya kiutambuzi yachangiayo kuleta mabadiliko ya lugha. Makala haya pia yamedhihirisha mchango na ufaafu wa vigezo vya kiutambuzi vya nadharia ya Semantiki Tambuzi katika kuelezea mabadiliko ya lugha.

Downloads

Published

30-04-2021

Issue

Section

Articles