Mabadiliko ya Utabaka

Ulinganishi wa Riwaya za 'Kuli' na 'Pendo la Karaha'

Authors

  • Virginia Wambui Mwathi Chuo Kikuu cha Machakos Author
  • Vifu Makoti Chuo Kikuu cha Machakos Author
  • John Mutua Chuo Kikuu cha Machakos Author

Keywords:

Utabaka, Tabaka, Ubepari, Nguvukazi

Abstract

Utabaka hudhihirika katika jamii ya kibepari ambayo hugawanya watu kulingana na uwezo wao wa kumiliki na kudhibiti njia za uzalishaji mali. Marx anadai kuwa, historia ya jamii ndiyo historia ya mgogoro wa matabaka. Kutawaliwa kwa watu wa tabaka la chini na wale wa juu kunaeleza jumla ya muundo wa jamii. Jamii ina tabia ya kubadilika kadri ya mpito wa wakati. Kutokana na sifa hii, makala hii itachunguza mabadiliko ya utabaka katika jamii ya kibepari kwa kulinganisha matukio ya kitabaka katika riwaya za Kuli (Shafi, 1979) na Pendo la Karaha (Habwe, 2014). Riwaya hizi zimeandikwa katika vipindi tofauti, Kuli imeandikwa katika karne ya 20 na Pendo la Karaha katika karne ya 21. Kwa hivyo, tunatarajia kuwa zitakidhi haja yetu ya kulinganisha ili kubaini ikiwa kuna mabadiliko yaliyokumba utabaka. Tunaamini kuwa utabaka ungalipo lakini kuna vipengele ndani yake vilivyobadilika kutokana na mpito wa wakati. Tutaongozwa na Nadharia ya Umarx iliyoasisiwa na Karl Marx na Friedrich Engels. Nadharia hii huonyesha migogoro ya kitabaka iliyopo katika jamii ambapo watu wa tabaka la chini hunyanyaswa na wale wa tabaka la juu. Tunatarajia kuwa utafiti huu utachangia katika fasihi ya Kiswahili na kuwa na umuhimu kwa wasomi katika viwango mbalimbali vya elimu na jamii kwa jumla.

Downloads

Published

30-04-2024

Issue

Section

Articles