Itikadi katika Riwaya za 'Dunia Yao' (2006) na 'Mhanga Nafsi Yangu' (2013) za S. A. Mohamed

Authors

  • Murithi Joseph Jesse Chuo Kikuu cha Kenyatta Author
  • Kitula King’ei Chuo Kikuu cha Kenyatta Author

Keywords:

Itikadi, Utandawazi, Mtazamo, Badilifu, Nyumbufu

Abstract

Makala haya yanaonesha kuwa itikadi ni dhana badilifu na nyumbufu kulingana na maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia. Itikadi ndiyo huelekeza misimamo, mielekeo na imani ya mtunzi na hivyo kuathiri mtazamo wa mwandishi kuhusu ulimwengu unaomzunguka, ambao huweza kubadilika kulingana na wakati na mahitaji ya kijamii. Katika mkabala huo makala haya yanatathmini itikadi ya mtunzi katika riwaya za Dunia Yao (2006) na Mhanga Nafsi Yangu (2013) za S. A. Mohamed. Kwa kutumia riwaya hizo, makala haya yanathibitisha kwamba itikadi ni dhana badilifu na nyumbufu na hutangamana na jinsi mtunzi anavyobadilisha mikakati yake ili kukidhi mahitaji ya jamii lengwa.

Downloads

Published

30-09-2019

Issue

Section

Articles