Mwanamke Dhidi ya Uanauke Wake katika Karne ya 21
Keywords:
Mwanamke, Nafasi ya Mwanamke, Ushairi, Mtazamo wa Kimapokeo, Mtazamo wa KisasaAbstract
Nafasi ya watunzi wa ushairi wanawake, katika ushairi wa Kiswahili inaendelea kukua kwa kiasi kikubwa. Mwanamke baada ya kuchorwa katika kazi mbalimbali za kifashi kwa mtazamo duni na watunzi wa kiume anawajibu wa kujitetea yeye mwenyewe. Makala haya yanalenga kutathmini mtazamo wa mshairi mwanamke juu ya mambo mbalimbali yanayomzunguka mwanamke katika maisha yake ya kila siku. Data za makala haya zilipatikana katika diwani ya Kurunzi ya mwandishi Rose Mbijima kwa mbinu ya usomaji makini. Matokeo yanaonesha kuwa mwanamke anapiga hatua kujiodoa kuwa mtu wa hadhi ya chini, kama ambavyo anachorwa katika kazi nyingi za kifasihi. Hata hivvyo, data zinaonesha kuwa Mwandishi Rose Mbijima anaendelea kumchora mwanamke kwa mtazamo hasi na wakimapokeo zaidi kuliko alivyomfunua kwa matazamo wa kisasa na chaya. Data zinadhihirisha kuwa yapo mambo kuhusu mapenzi na ndoa ambayo mtunzi anamtazamo wa kimapokeo kama zilivyo jamii nyingi za kiafrika. Aidha, kuhusu mtazamo chanya na wakimapinduzi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii yake, mwanamke ameonekana akipaza sauti na kutoa maoni yake. Makala haya, yanahitimisha kwa kutoa mapendekezo kuwa, watunzi wa kike wa ushairi wapewe majukwaa mengi zaidi ili waweze kuwasilisha kazi zao, hali ambayo itaendelea kuchochea mabadiliko makubwa ya wanawake juu ya mtazamo wao kuhusu uanauke wao na jamii kwa ujumla kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii.
References
Challigha, N. E. (2011). Usawiri wa Mwanamke na Mgawanyo wa Majukumu Kijinsia katika Fasihi Picha ya Katuni Mnato za Kiswahili. Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Indede, F. (2011). Mwanamke Angali Tata Katika Ushairi wa Kisasa? Swahili Forum, 18, 163-197.
Lyatuu, J. (2011). Usawiri wa Wanawake katika Fasihi ya Kiswahili: Ulinganifu wa Waandishi wa Kike na Kiume: Uchaguzi katika Riwaya Teule. Tasinifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mbijima, R. (2019). Kurunzi. Dar es Salaam: Moccony Printing Press.
Mwakanjuki, N. (2022). Mapungufu ya Kiutamaduni Yanavyoathiri Ustawi wa Mwanamke katika Jamii: Mifano Kutoka Riwaya ya Sikujua. Jarida la Fahari ya Kiswahili, 1(1), 115-130.
Ngaiza, M. K. (2004). Harmonization and Mainstreaming Gender in Local Government or Transforming Patriarchy: The Case of Two Wards in Bukoba District Council, Tanzania. Tanzanian Journal of Development Studies, 5, 25-38.
Ponera, A. S. (2014). Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi. Dar es Salaam: Karljamer Print Technology.
Rodney, W. (1972). How Europe Underdeveloped Africa. London: Rogle-L’Ouverture Publishers.
Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Open University Press.