Nafasi ya Fasihi ya Watoto katika Ukuzaji wa Mshikamano wa Kitaifa
Keywords:
Fasihi ya Watoto, Mshikamano, UtangamanoAbstract
Fasihi ya watoto ni aina ya sanaa ambayo imeandaliwa kwa ajili ya watoto. Fasihi hii inaweza kuwa imetungwa na kuandikwa na mtu mzima au mtoto, na hulenga watoto kama hadhira teule. Sanaa hii huhusisha tanzu nyingi ambazo zinawapa watoto nafasi za utendaji. Fasihi ya watoto ina tanzu anuai nazo ni nyimbo na ushairi, michezo ya kuigiza, hadithi, mchongoano na misemo miongoni mwa nyingine. Wakati wa utendaji, watoto hujumuika na wenzao ili kutekeleza utanzu wowote. Wanapojumuika pamoja, watoto huonyesha ushirikiano wao kupitia ugawanyaji wa majukumu, vifaa vya kuchezea, uongozi wa nyimbo na kuwakinga wenzao dhidi ya madhara yoyote. Wanapofanya hivyo, watoto hukuza umoja na mshikamano baina yao. Wakati wa kuimba kwa mfano, watoto huimba kwa zamu ili kila mmoja ahisi kuthaminiwa na wenzake. Ni kwa msingi huu ndipo makala haya yanapambanua nafasi ya fasihi ya watoto katika ukuzaji na uendelezaji wa mshikamano wa kitaifa na utangamano.