Sababu za Mkengeuko wa Malezi kwa Wahusika katika Riwaya ya 'Rosa Mistika'

Authors

  • Selestino Helman Msigala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Riwaya, Kukengeuka, Malezi, Nadharia ya Sosholojia

Abstract

Ingawa wahusika hukengeuka malezi, wataalamu na wachambuzi hutofautiana katika kuelezea jambo hili. Wapo wanaoona kuwa, kukiuka malezi kwa wahusika katika kazi za fasihi kunasababishwa na wazazi au walezi (Wanjala, 2015; Mbatiah, 2016; Doepke na Zilibotti, 2019). Kwa upande mwingine, wapo wataalamu wanaowatupia lawama watoto kuwa wanabadilika hasa wanapotoka mikononi mwa wazazi na kuingia katika jamii kutokana na kushindwa au kupuuza malezi na maelekezo kutoka kwa wazazi au walezi wao (Ondieki, 2015; Jonas, 2017). Aidha, upande mwingine jamii hulaumiwa kwa kushindwa kuendeleza malezi yanayofaa kutoka kwa wazazi au walezi wa watoto (Mitchell, 2010; Martin, 2017; Sanga, 2018). Tofauti hizi za kimtazamo ndizo zilizosukuma kuandikwa kwa makala hii. Kwa hivyo, makala hii inakusudia kujadili sababu za mkengeuko wa malezi kwa wahusika kwa kutumia riwaya ya Rosa Mistika (Kezilahabi, 1971).

Downloads

Published

30-04-2024

Issue

Section

Articles