Ubainishaji wa Viashiria vya Kiujumi katika Riwaya ya Kiswahili

Uchunguzi wa Riwaya Teule za Kimajaribio

Authors

  • Festo Joster Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author
  • Elizabeth Mahenge Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Ujumi, Vijenzi vya Kiujumi, Viashiria vya Kiujumi, Mwitiko

Abstract

Makala haya yanabainisha viashiria vya kiujumi katika riwaya ya Kiswahili yakijiegemeza katika riwaya teule za kimajaribio. Msukumo wa kushughulikia viashiria vya kiujumi katika riwaya ya Kiswahili ya kimajaribio unatokana na kuwapo kwa madai kuwa riwaya za mkondo huu kama vile Nagona (1990) na Mzingile (1991) za Kezilahabi hazina maana katika jamii ya Afrika Mashariki (Mbatia, 1998). Hii ina maana kuwa riwaya za mkondo huu hazina ujumi wowote katika kuleta maendeleo kwa jamii ya Afrika Mashariki. Riwaya kuwa na maana huanzia katika sababu za kuandikwa kwake Jones (1994). Kutokana na mpishano huo wa mawazo, tuliona ipo haja ya kuchunguza ujumi wa riwaya hizi za kimajaribio ili kubainisha viashiria vya kiujumi katika riwaya za Kiswahili. Ili kufikia matokeo ya utafiti huu riwaya teule mbili yaani Bina-Adamu! (2002) ya Wamitila na Dunia Yao (2006) ya Mohamed zilihakikiwa. Data kutoka uwandani zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji, mijadala ya vikundi na usaili. Data zilitoka kwa watoa taarifa wasomaji ambao ni wanafunzi wa Shahada ya Awali na Umahiri katika Kiswahili kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile wandishi wa riwaya husika kutoka Nairobi Kenya na Wete Pemba walihusika kutupatia data. Makala yaliongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Kiujumi. Kwa kutumia mkabala wa kitaamuli tulichambua, tulichakata na kuwasilisha data. Matokeo yanaonesha kwamba riwaya za Kiswahili za kimajaribio zina viashiria vya kiujumi ambavyo vinadhihirisha ujumi wa riwaya hizi. Ujumi huo una mchango mkubwa sana katika firka za wasomaji kwa maendeleo ya Afrika Mashariki. Aidha, makala haya yanatia chachu kwa tafiti nyingine kuchunguza mbinu zinazowasaidia waandishi na wahariri kuukamilisha ujumi wa riwaya hizi.

Downloads

Published

30-04-2022

Issue

Section

Articles