Mchakato wa Uandishi Bunifu kama Unavyoakisiwa katika Riwaya za Kisasa za K.W. Wamitila

Authors

  • Janice M. Mutua Chuo Kikuu cha Egerton Author
  • Issa Mwamzandi Chuo Kikuu cha Kabianga Author
  • AbdulRahim Taib Chuo Kikuu cha Kabianga Author

Keywords:

Kariha, Riwaya za Kisasa, Mwandishi, Uandishi bunifu, Mhariri, Mchapishaji

Abstract

Makala haya yamejibana katika ufafanuzi wa upekee wa mtunzi wa riwaya za Kiswahili za kisasa pamoja na changamoto anazopitia mikononi mwa wahariri na wachapishaji kama inavyopendekezwa katika riwaya zenyewe. Aidha, makala imependekeza njia za kuboresha na kukuza riwaya mpya za Kiswahili. Madhumuni yake ni kufafanua mchakato mzima wa uandishi wa riwaya mpya kwa kuwaangazia wahusika watatu muhimu yaani mwandishi, msomaji na mchapishaji. Nadharia ya usasaleo imeuongoza mjadala huu katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Mintarafu ya nadharia, mtunzi wa kazi bunifu ana uhuru wa kuandika jinsi apendavyo, hailazimu kwamba riwaya zifuate utaratibu mahususi. Mkabala wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kuchanganua data iliyohusiana na swala zima la ubunifu na uchapishaji wa riwaya mpya ya Kiswahili. Data ilichanganuliwa kwa kuangazia maudhui na vipengele vya mbinu za kimajaribio kama vile dayolojia, urejeleomatini, simulizi fupi na taashira. Riwaya za Mwandishi, Msomaji na Mchapishajii na Musaleo! zimetumika kuangazia mchakato huuMatokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Imebainika kuwa sura na ubunifu wa riwaya mpya ni zao la usomi. Ili kuelewa ujumbe katika riwaya za kisasa ni muhimu kwa ‘mhariri’ kufanya utafiti wa kina kabla ya kutoa mapendekezo yake kwa mchapishaji. Aidha, inailazimu hadhira kuwa na ufahamu wa mambo mengi kiada ili kung’amua yanayowasilishwa katika riwaya za kisasa.

Downloads

Published

30-09-2021

Issue

Section

Articles