Changamoto Zinazoathiri Matumizi ya Filamu za Kibongo zenye Tafsiri katika Ufundishaji wa Msamiati wa Kiswahili kwa Wageni

Authors

  • Julius Matovu Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, UDSM Author
  • Pendo Salu Malangwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, UDSM Author

Keywords:

Tafsiri, Filamu za Kibongo, Msamiati, Kiswahili na Wageni

Abstract

Makala haya yamechunguza changamoto zinazoathiri matumizi ya filamu za Kibongo zenye tafsiri katika ufundishaji wa msamiati wa Kiswahili kwa wageni nchini Tanzania. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Ujifunzaji kwa njia ya Media Anuwai ya Mayer (2009). Uchambuzi wa data za utafiti huu umetumia mkabala wa kitaamuli na mbinu ya kuchambua maudhui. Data za utafiti huu zilipatikana kutoka katika vituo vitatu vinavyofundisha Kiswahili kwa wageni ambavyo ni Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Kiswahili na Utamaduni (KIU) na Kituo cha Mafunzo ya Ushirikiano na Maendeleo ya Kimataifa (MS-TCDC). Data za makala haya ni sehemu ya data zilizokusanywa kwa ajili ya shahada ya umahiri[1] ya mwandishi wa makala haya akishirikiana na msimamizi wake ambaye ni mwandishi mwenza wa makala haya. Mbinu za usaili na ushuhudiaji zilitumika kukusanya data kutoka kwa walimu tisa wanaofundisha Kiswahili kwa wageni. Matokeo ya utafiti huu yameonesha changamoto mbalimbali zinazoathiri matumizi ya filamu za Kibongo zenye tafsiri katika ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni. Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa vitendeakazi, filamu kuchukua muda mwingi wa kipindi, filamu kuwa na makosa kwenye tafsiri zake, changamoto ya utamaduni, filamu kwenda kwa kasi, mtazamo hasi wa wanafunzi na changamoto ya umeme. Utafiti huu umependekeza kwamba vituo vinavyofundisha Kiswahili kwa wageni viboreshe mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

 

[1] Kukamilika kwa shahada hiyo ni kutokana na ufadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Mchango wao tunautambua na kuuthamini sana.

Downloads

Published

30-09-2023

Issue

Section

Articles