Nafasi ya Tafsiri katika Ufundishaji wa Kiswahili: Mfano wa Ufundishji wa Kiswahili katika Shule za Upili nchini Uganda
Keywords:
Tafsiri, Ufundishaji, Ujifunzaji, Kiswahili, UgandaAbstract
Makala haya yanaangazia maoni ya walimu na wajifunzaji kuhusu matumizi ya tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji Kiswahili katika shule za upili nchini Uganda. Suala mojawapo linalozua mgogoro miongoni mwa wasomi, wataalamu, walimu na wajifunzaji wa lugha ni matumizi ya tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kigeni na ya pili. Wanafunzi walioshiriki walikuwa wa kidato cha kwanza na cha pili. Data ilichanganuliwa kwa kutumia nadharia ya umotishaji wa lugha iliyoasisiwa na Gardner (1985) na kuendelezwa na Dörnyei (1994). Matokeo yanaonesha kwamba tafsiri ina nafasi kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili katika shule za upili nchini Uganda. Aidha, imebainika kwamba tafsiri haiwezi kuepukika katika mazingira ya ufundishaji wa Kiswahili nchini Uganda. Hata, hivyo mbinu hii inapaswa kutumika pamoja na mbinu nyinginezo na kwa njia inayofaa.