Tafsiri ya Chata za Huduma
Nafasi ya Kukuza Msamiati na Istilahi za Kiswahili
Keywords:
Chata za Huduma, Tafsiri, Ukuzaji wa Msamiati, Istilahi za KiswahiliAbstract
Tangu kuzinduliwa kwa Katiba ya Kenya ya mwaka 2010, mashirika mbalimbali yamejihimu kutafsiri baadhi ya nyaraka zake kuu katika Kiswahili kutoka Kiingereza. Miongoni mwa nyaraka hizi ni chata za huduma. Chata ya huduma ni hati inayotaarifu umma kuhusu huduma zinazotolewa na asasi, idara ama shirika fulani mahususi; viwango vya huduma vinavyotarajiwa na jinsi wateja wanavyoweza kuwasilisha maoni ama malalamishi yao kwa lengo la kuboresha huduma hizo. Tathmini ya tafsiri za chata hizi za huduma inasawiri tafsiri hizi kama nafasi ya kukuza na kupanua msamiati na istilahi za Kiswahili hasa kutokana na umahususi wa kitaaluma. Katika makala haya, tunaangazia ndaro na changamoto katika tafsiri ya baadhi ya istilahi zinazotumiwa katika mashirika mbalimbali. Tunahoji kwamba huu unaweza kuwa mwanzo wa kukita istilahi na msamiati au kupanua matumizi ya baadhi ya maneno kuafikia msamiati na istilahi hizi mpya.