Filamu ya Kiswahili

Fasihi Simulizi Iliyostawi

Authors

  • Gervas A. Kasiga Chuo Kikuu cha Dodoma Author
  • Neema Julius Luhwago Chuo Kikuu cha Dodoma Author

Keywords:

Filamu, Tamthiliya, Drama, Drama ya Runinga

Abstract

Makala haya yanaijadili sanaa ya filamu za Kiswahili kama fasihi simulizi iliyopevuka na kuchukua mkondo wa kiteknolojia kutokana na utegemezi wake wa nyenzo za kisasa katika utambaji. Hadhi ya kisanaa ya filamu imetazamwa kwa namna inayoonesha kujitokeza kwake kupitia umbo na wajihi wa kifasihi. Filamu imeonekana kuwa jukwaa huru linaloruhusu sanaa tofauti zinazosindikiza ujenzi wa maudhui ya kifasihi kujipenyeza kusaidia kuutengeneza ujumi wa kifasihi. Kustawi kwa fasihi simulizi kupitia umbo la filamu kumechunguzwa kwa namna inavyodhihirisho taswira zilizo ndani ya bongo la mtambaji: anayezitoa na kuziweka katika picha jongefu ili mtazamaji azione runingani na kumfanya ayaone maumbo ambayo alipaswa kuyafasiri kulingana na mwendelezo wa simulizi. Ukuaji wa filamu ya Kiswahili umejadiliwa sanjari na udondokaji wa usomaji wa riwaya, tamthiliya, pamoja na ushukaji wa jumla wa kusoma nchini Tanzania. Licha ya filamu kuonekana kupiga kasi katika kueneza Kiswahili, ukuzaji wake umeonekana kutia shaka. Hivyo, imeonekana ni vyema somo la uandishi wa filamu liingizae katika mtalaa wa fasihi ya Kiswahili ili kuwajenga waandishi wa miswada ya filamu pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa wanaKiswahili. Mwishoni, manju wa fasihi simulizi ya Kiswahili wameshauriwa kuchangamkia kukua kwa teknolojia kimawasiliano na kiuhifadhi wa sanaa, fasihi na utamaduni.

Downloads

Published

01-09-2020

Issue

Section

Articles