Mikakati Inayopendekezwa na Euphrase Kezilahabi katika Kukabiliana na Dhana Potofu Zilizopandikizwa na Wageni kuhusu Afrika na Mwafrika

Authors

  • Alfred Malugu Chuo Kikuu cha Rongo Author
  • Ernest Sangai Mohochi Chuo Kikuu cha Kibabii Author
  • Mugyabuso Mlinzi Mulokozi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Historia, Dhana Potofu, Afrika, Mwafrika, Mikakati, Ubaadaukoloni

Abstract

Suala la dhana potofu kuhusu Afrika na Mwafrika lina historia ndefu sana. Historia yake inaweza kutazamwa kuanzia kipindi cha ukoloni. Dhana hizo potofu kuhusu Afrika na Mwafrika zilijengewa msingi wake sio tu katika vitabu vya dini kama vile Biblia Takatifu, bali pia kwa wanafalsafa na wasomi maarufu wa kale wa Kimagharibi kama vile Carl Meinhof na Georg Hegel. Dhana potofu zilizopandikizwa zilichochea kutawaliwa kwa Waafrika na Afrika kwa jumla. Kwa mfano, kwa kupitia Biblia Takatifu kuna hoja kuwa masaibu, shida, majanga na mambo mbalimbali yanayomsibu Mwafrika yanatokana na kulaaniwa. Kutokana na kuwapo kwa dhana potofu, makala hii inakusudia kutathmini mikakati mbalimbali inayopendekezwa na Euphrase Kezilahabi katika kukabiliana na dhana hizo. Mikakati hiyo itabainishwa kupitia riwaya za Kezilahabi za Gamba la Nyoka, Nagona na Mzingile. Aidha, katika kubainisha dhana hizo, tutaongozwa na baadhi ya mihimili ya Nadharia ya Ubaadaukoloni. Hii ni Nadharia inayofungamanishwa na Edward Said hususani baada ya kuandika kitabu chake cha Orientalism (1978).

Downloads

Published

30-04-2022

Issue

Section

Articles

How to Cite

Mikakati Inayopendekezwa na Euphrase Kezilahabi katika Kukabiliana na Dhana Potofu Zilizopandikizwa na Wageni kuhusu Afrika na Mwafrika. (2022). Mwanga Wa Lugha, 7(1), 61-76. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/262