Usemezanoghaibu katika Diwani ya 'Kimbunga'

Authors

  • Mohammed Soud Juma Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Author

Keywords:

Usemezanoghaibu, Diwani, Kimbunga, Usemazano

Abstract

Makala haya imekusudia kushughulikia usemezanoghaibu unaojitokeza katika diwani ya Kimbunga, iliyoandikwa na Haji Gora. Aidha, makala imejikita katika kuangalia aina za usemezano uliotumika katika mashairi ya msanii huyo. Pia, makala inaonesha aina mpya ya usemezano iliyotumiwa na msanii huyu, kinyume na aina zile zilizoorodheshwa na Bakhtin juu ya aina za usemezano zinazotumika katika riwaya na kuonesha uwezekano wa kutumika kwa usemezano na usemezanoghaibu katika uga mwengine wa fasihi kinyume na riwaya peke yake. Hivyo, makala inaonesha kutumika kwa usemezano katika ushairi wa Kiswahili na kuibuka kwa usemezanoghaibu, kuwa ni dhana mpya ya usemezano inayopatikana kwa wasanii wa fasihi hasa wasanii wa ushairi. Katika makala haya inapendekezwa kufanyike kwa utafiti mwengine kwa kuitumia dhana ya usemezanoghaibu na kuzama ndani zaidi ili kuweza kugundua mambo mapya yanayotumiwa na wasanii.

Downloads

Published

30-09-2022

Issue

Section

Articles