Tathmini ya Matumizi ya Istilahi za Kitehama kwa Wazungumzaji wa Kiswahili

Mifano Kutoka kwa Watumiaji wa Simu nchini Tanzania

Authors

  • Majura Nyangaywa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Author
  • Pendo S. Malangwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Tathmini, Matumizi, TEHEMA, Istilahi

Abstract

Makala haya yanaangazia hali ya matumizi na kukubalika kwa istilahi za kitehama za Kiswahili za simu za mkononi miongoni mwa wazungumzaji wa Kiswahili nchini Tanzania. Data za uwandani zilikusanywa kutoka kwa watoa taarifa 68 katika kata za Kimara na Ubungo, Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam, Tanzania. Data zilikusanywa kwa mbinu ya usomaji wa matini, hojaji na usaili. Nadharia ya Ulinganifu wa Kiathari ilitumika kuongoza utafiti huu. Matokeo ya utafiti yamechambuliwa kwa mkabala wa kitaamuli na kitakwimu. Matokeo ya tathmini yanaonesha kuwa, upokelewaji wa istilahi za Kiswahili za programu za simu za mkononi, una mambo mchanganyiko miongoni mwa wazungumzaji wa Kiswahili. Baadhi ya istilahi zinakubaliwa na nyingine ama hawazielewi au hawazikubali. Wanaikubali istilahi hizo, wanatoa sababu mbalimbili zikiwemo urahisi na uelewekaji wa istilahi za Kiswahili. Sababu nyingine ni ugumu wa istilahi za Kiingereza zilizopo katika programu za simu. Kwa upande mwingine, sababu zinazowafanya baadhi ya watumiaji wa simu kutozikubali istilahi za Kiswahili wanaona kuwa, ni ushamba kutumia Kiswahili kwenye simu iliyowekewa Kiingereza tayari. Pia, wanaiona lugha ya Kiingereza kuwa ni lugha ya Kimataifa. Hivyo, makala haya yanapendekeza kwamba, kuna haja ya kutathmini michakato ya uundaji wa istilahi za programu za simu, kuwashirikisha watumiaji wa simu wanaozungumza Kiswahili ili kuunda istilahi kubalifu.

Downloads

Published

30-09-2022

Issue

Section

Articles