Uhusiano Mwema kati ya Mke na Mume kama Njia ya Kudumisha Ndoa

Mifano kutoka 'Utendi wa Ayubu'

Authors

  • Angela Sawe Chuo Kikuu cha Kabarak Author
  • Vifu Makoti Chuo Kikuu cha Machakos Author
  • S. M. Obuchi Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Uhusiano, Mke, Mume, Ndoa, Utendi wa Ayubu

Abstract

Makala haya yanahusu uhusiano wa mke na mume katika ndoa kwa kuangazia Utendi wa Ayubu (UWA). Utendi huu, unamhusu Mtume mwaminifu wa Mungu aitwaye Ayubu aliyebarikiwa na mali nyingi sana. Alikuwa mcha Mungu na aliyeimarika kwa imani yake. Kutokana na imani hii na baraka nyingi alizokuwa nazo, shetani anamwonea wivu. Shetani anamwomba Mungu ruhusa ili aweze kumjaribu Ayubu. Aliporuhusiwa na Mungu, shetani anamfilisi na kumdhuru kiafya lakini Ayubu anasimama imara katika imani yake na wala hakumkana Mungu. Kwa upande mwingine, Rehema mkewe anaibuka kama mwanamke mnyenyekevu, mwaminifu na anayependa mumewe kwa dhati.

Downloads

Published

30-09-2018

Issue

Section

Articles