Matumizi ya Usambamba kama Nduni ya Kimtindo katika Kuibua Maudhui ya Dini katika Riwaya ya 'Paradiso'

Authors

  • Victor Kyomuhendo Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Mosol Kandagor Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Samuel M. Obuchi Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Dini, Mtindo, Paradiso, Uchimuzi, Usambamba

Abstract

Makala haya yanachunguza matumizi ya usambamba kama nduni ya kimtindo katika kuibua maudhui ya dini katika riwaya ya Paradiso. Tunachunguza miundo mbalimbali ya kiusambamba iliyotumika katika riwaya hiyo kuibua maudhui ya dini. Suala la dini ni la msingi katika jamii mbalimbali kwa vile dini imeshikamana na maisha ya kawaida ya wanajamii. Ndani ya mada ya jumla ya dini, riwaya hii inaangazia dhamira zinazoathiri jamii kama vile ufisadi na ujilimbikiziaji mali, ufungamano wa siasa na dini, pamoja na masuala ya kijinsia. Tulidondoa vifungu kutoka katika riwaya hiyo kwa mkono kwa sababu haipatikani kielektroniki. Data iliteuliwa kimaksudi kwa kulenga maudhui yanayohusu suala la dini. Katika ukusanyaji na uchambuzi wa data tumetumia Nadharia ya Uchimuzi. Orodha ya kategoria za kiisimu na kimtindo ya Leech na Short (2007) ilitumiwa kubainisha ngazi kuu za uchunguzi wa kimtindo. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kwamba usambamba ni njia kuu aliyoitumia mwandishi kuibulia na kusisitizia maudhui kuhusu dini. Usambamba huu unajitokeza katika ngazi za virai na vishazi na unahusisha aina mbalimbali kama vile anafora, epifora, tanakuzi na mjalizo. Usambamba wa aina ya anafora ndio umedhihirika zaidi katika riwaya ya Paradiso. Makala haya yanapendekeza kwamba usambamba wa kisintaksia unafaa kuhusianishwa na usambamba wa kileksika katika kuzichambua kazi za kifasihi za Kiswahili kimtindo.

References

Galperin, I. R. (1977). Stylistics (2nd Ed.) Moscow: Vishaya Shkola.

Habwe, J. (2005). Paradiso. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation.

Jeffries, L. & McIntyre (2010). Stylistics. United Kingdom: Cambridge University Press.

Kazungu, K. (1982). Deviation and Foregrounding in Chosen Literary Texts [Unpublished Master’s dissertation]. University of Nairobi.

Kipacha, A., & Jilala, H. (2021). Nadharia za Elimumitindo ya Kiswahili. Dar es Salaam: Daud Publishing Company Ltd.

Kitsao, J. (1975). A Stylistic Approach Adopted for the Study of Written Swahili Prose Texts (Unpublished Master’s Dissertation). University of Nairobi.

Kitsao, J. (1982). An Investigation of Themes in Swahili Literature and An Application of Stylostatistics to Chosen Texts. Tasnifu ya Uzamifu ya Chuo Kikuu cha Nairobi.

Leech, G., & Short, M. (2007). Style in Fiction (2nd Ed.). United Kingdom: Pearson Education Limited.

Massamba, D. P. B., et al., (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA). Dar es Salaam: TUKI.

Massamba, D. P. B. (2004). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

Mbatiah, M. (2001). Kamusi ya Fasihi. Nairobi: Standard Textbooks, Graphics and Publishing.

Michira, J. N. (2018). A Stylistic Analysis of John Habwe’s Pendo la Karaha. International Journal of Humanities and Social Sciences, 6(6).

Short, M. (2013). Exploring the Language of Poems, Plays and Prose. New York: Routledge.

Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publications Ltd.

Downloads

Published

30-04-2025

Issue

Section

Articles

How to Cite

Matumizi ya Usambamba kama Nduni ya Kimtindo katika Kuibua Maudhui ya Dini katika Riwaya ya ’Paradiso’. (2025). Mwanga Wa Lugha, 10(1), 111-118. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/550

Most read articles by the same author(s)

Similar Articles

1-10 of 22

You may also start an advanced similarity search for this article.