Mchango wa Wanawake wa Kiswahili katika Uongozi, Dini na Ushairi 1350 B.K-1840 B.K.

Authors

  • Kineene wa Mutiso Chuo Kikuu Nairobi Author

Keywords:

Wanawake, uongozi, dini, ushairi

Abstract

Wataalamu wengi wa fasihi ya KiSwahili hawajui kwamba kuna washairi wengi wa KiSwahili wa kike, ambao wamechangia sana katika tasnia hii. Mshairi maarufu anayejulikana na wengi ni Mwana Kupona binti Mshamu. Ni wachache zaidi wanaojua hata kiongozi mmoja mashuhuri wa kike. Katika makala haya, nimeangalia mchango wa washairi na viongozi wa kike wa KiSwahili, wa upwa wa mwambao wa Afrika Mashariki na visiwani. Kwa kutoa ithibati za kimapisi na kiushairi, nathibitisha kwamba wanawake wa KiSwahili wamekuwa katika mstari wa mbele kiutunzi, kidini, kimapisi na kiuongozi, kwa muda mrefu sana. Wameshughulikia sio tu waadhi na mapenzi, mbali pia yale waandishi kwa kiume wa KiSwahili wameshughulikia. Nimejikita kati ya mwaka 1350 B.K na 1810 B.K. Nimeonyesha kwamba ni baada ya majilio ya watawala wa kigeni ambapo mwanamke wa KiSwahili alizidi kukandamizwa, kwa sababu za kidini, kitamaduni na kikoloni. Wa aidha, nimedhibitisha kwamba washairi na viongozi hawa wa kike walipatikana sio katika sehemu moja tu, bali katika upwa mzima na visiwani.

Downloads

Published

30-04-2019

Issue

Section

Articles