Usawiri wa Masuala Mbalimbali ya Kiuhalisia-Hakiki katika Riwaya za 'Kichwamaji' na 'Dunia Uwanja wa Fujo' za Euphrase Kezilahabi

Authors

  • Tusingwire Timon Chuo Kikuu cha Kabale Author
  • Flavian Ilomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Uhalisia Hakiki, Kichwamaji, Dunia Uwanja wa Fujo, Kuchambua, Kukosoa

Abstract

Uhalisia-hakiki ni mtindo wa uandishi ambao mwandishi hushambulia maovu ya jamii bila kuogopa. Katika mtindo huu, mwandishi huchambua maovu yaliyopo kwenye jamii na kuyaweka wazi bila kificho. Hata hivyo, ni waandishi wachache wenye uthubutu huo hasa kama maovu hayo yanawahusu wenye mamlaka moja kwa moja. Makala haya yamechunguza masuala yaliyosawiriwa kiuhalisia hakiki katika riwaya za Kichwamaji na Dunia Uwanja wa Fujo zilizoandikwa na Euphrase Kezilahabi mwaka 1974 na 1975 mtawalia. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini teule. Katika kudhihirisha masuala hayo tuliongozwa na Nadharia ya Uhalisia kwa kujikita katika Mkabala wake wa Uhalisia Hakiki. Mkabala huu umejengeka katika wazo kuwa, waandishi wa kiuhalisia hakiki hawaishii tu kusawiri hali kama ilivyo katika jamii, bali huchambua, hukosoa na kusaili hali hizo yameonesha kwamba, masuala ya kiuhalisia hakiki yanayodhihirika kwenye riwaya hizo ni kifo, uwepo wa Mungu, maana ya maisha, uhuru wa mwandamu, na ukahaba.

References

Arabi, S., Moghbel, A. G., Zareh, N., Balawi, R., na Pourabed, M. J. (2022). A Comparative Study of the Aspects of Critical Realism between Yiki Boud Yaki Nabud of Muhammad Ali Jamalzadeh and Kan Ma Kan by Mikhail Naima. Biannual Journal. Inapatikana katika https://doi.org/10.30465 /afg.2022.6771. Ilisomwa tarehe 10 Januari 2023.

Badru, Z. A. (2019). Uchunguzi wa Fumbo la Uhuru wa Mtu: Mifano kutoka Riwaya za Euphrase Kezilahabi. Katika A. S. Ponera na Z. A. Badru (Wah.), Koja la Taaluma za Insia: Kwa Heshima ya Profesa Joshua S. Madumulla (481-507). Dar es Salaam: Karljamer Publishers Limited.

Duwe, M. (2020). Usawiri wa Eskatolojia ya Waafrika katika Mbolezi za Wangoni. Jarida la CHALUFAKITA, 2, 158-173.

Gorky, M. (1949). Mother. Moscow: Progress Publishers.

Kezilahabi, E. (1974). Kichwamaji. Nairobi: Vide~Muwa Publishers.

Kezilahabi, E. (1975). Dunia Uwanja wa Fujo. Nairobi: Vide~Muwa Publishers.

Khalid, K. (1982). The Prostitute in Progressive Literature. London: Allison and Busby.

Madumulla, J. S. (2009). Riwaya ya Kiswahili; Nadharia, Historia na Misingi ya Uchambuzi. Dar es Salaam: Mture Educational Publishers Limited na Nairobi: Phoenix Publishers Limited.

Mbiti, J. S. (1969). African Religious and Philosophy. Nairobi: East African Educational Publishers Limited.

Mlacha, S. A. K. na Madumulla, J. S. (1991). Riwaya ya Kiswahili. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.

Mulokozi, M. M. (2017). Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: KAUTTU.

Odongo, O. F. (2014). Uchanganuzi wa Uwasilishaji wa Kifo katika Mashairi Teule ya Kiswahili. Tasnifu ya Umahiri (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Maseno, Kisumu.

Quayson, A. (2000). Postcolonialism: Theory, Practice or Process. Cambridge: Polity Press.

Raphael, D. (2018). Usawiri wa Ontolojia ya Kiafrika katika Ngano za Kiha. Tasnifu ya Umahiri (Haijachapishwa). Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam.

Sanga, T. J. (2020). Dhima za Mbolezi za Sasa katika Jamii ya Wakinga Waishio Makete, Tanzania. Kioo cha Lugha, 18, 208-228.

Sivananda, S. S. (1997). What Become of the Soul After Death. Himalayas: The Devine Life Society.

TUKI. (2019). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.

Wamitila, K. W. (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Vide~Muwa Publishers.

Downloads

Published

30-04-2025

Issue

Section

Articles

How to Cite

Usawiri wa Masuala Mbalimbali ya Kiuhalisia-Hakiki katika Riwaya za ’Kichwamaji’ na ’Dunia Uwanja wa Fujo’ za Euphrase Kezilahabi. (2025). Mwanga Wa Lugha, 10(1), 35-47. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/543

Similar Articles

11-20 of 227

You may also start an advanced similarity search for this article.