Miundo ya Viegesho vya Kiwango katika Sentensi za Kiswahili
Mtazamo wa Nadharia ya Eksibaa
Keywords:
Miundo, Viegesho, Sentensi, EksibaaAbstract
Makala yanahakiki viegesho vya kiwango katika sentensi za Kiswahili. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, usaili, ushuhudiaji na usomaji matini ambazo zilihusu ubainishaji wa viegesho vya kiwango. Nadharia ya Eksibaa iliyoasisiwa na Chomsky (1970) imetumiwa kubainisha na kuchambua miundo ya viegesho hivyo. Data zimechanganuliwa kwa kutumia mbinu ya vielelezo vya mchoroti pamoja na maelezo. Matokeo yanadhihirisha kuwa kisintaksia, kuna miundo kumi na nne (14) ya viegesho vya kiwango katika sentensi za Kiswahili. Miundo hiyo imetokana na ushikamani wa viambajengo vinavyounda viegesho vya kiwango katika Kiswahili.