Fasihi Simulizi kama Nyenzo Muhimu katika Taaluma ya Kitabibu (Afya)

Authors

  • Neema Julius Luhwago Chuo Kikuu cha Dodoma Author

Keywords:

Fasihi Simulizi, Nyenzo, Taaluma ya Kitabibu

Abstract

Makala haya yanakusudia kueleza jinsi fasihi simulizi ilivyo nyenzo muhimu katika taaluma ya kitabibu kwenye uelimishaji wa jamii na kutahadharisha kuhusu magonjwa Kama vile UKIMWI, UVIKO-19, Kaswende, Kisonono, Hepatitis B (Homa ya Ini B), Saratani, Kifua kikuu na Malaria. Aidha, yatajenga msingi wa ushirikiano baina ya wanataaluma wa Fasihi simulizi na wataalamu wa sekta ya afya katika utekelezwaji wa mpango wa Sera ya maendeleo na ustawi wa jamii. Si hivyo tu, bali yatasaidia kutanua wigo wa taaluma ya fasihi kuanza kutoa mwanga kwa wanataaluma na wadau wote wa fasihi simulizi kuzimulikia taaluma mbalimbali zilizopo kwenye jamii na jinsi zinavyoweza kuhusiana na fasihi katika ustawishaji wa maendeleo ya jamii husika. Pia kuitazama fasihi simulizi kwa jicho jipya linaloendana na kipindi tulichonacho cha maendeleo ya sayansi na teknolojia. Vilevile katika kuutazama mustakabali wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili na fasihi yake kwa jumla, tunataraji kuona ushirikiano thabiti kati ya sekta ya afya na fasihi simulizi katika utoaji wa elimu zihusuzo kinga na afya kwa jamii ya nchi zote za Afrika Mashariki.

References

Hann, C. (2021). One Hundred Years of Substantivism Economic Anthropology.

https://www.google.com/search?q=TAALUMA+YA+UTABIBU+PDF&ie=utf-

Mrikaria, S. (2007). Fasihi Simulizi na Technology Mpya. Swahili Forum, 14, 197 – 2006.

Mulokozi, M. M. (1983). Utafiti wa Fasihi Simulizi. Makala ya Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili III: Fasihi. Dar es Salaam: TUKI, 1-25.

Mulokozi, M. M. (1996). Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Mushengezi, A. (2003). Twentieth Century Literary Theory. Kampala: Makerere University.

Njogu, K., & Wafula, R. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

Okphewho, I. (1992). African Oral Literature. USA: Indiana University Press.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hotuba ya Waziri wa Afya

TUKI. (2003). Fasihi. Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili. Dar-es-Salaam: TUKI.

TUKI. (2007). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: Oxford University Press.

Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation,.

Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Downloads

Published

30-09-2024

Issue

Section

Articles

How to Cite

Fasihi Simulizi kama Nyenzo Muhimu katika Taaluma ya Kitabibu (Afya). (2024). Mwanga Wa Lugha, 9(2), 45-51. https://journals.mu.ac.ke/index.php/mwl/article/view/531

Similar Articles

41-50 of 198

You may also start an advanced similarity search for this article.