Athari za Kifonolojia za Lugha za Kinailotiki kwa Kiswahili

Mifano kutoka Kenya

Authors

  • James Omari Ontieri Chuo Kikuu cha Maasai Mara Author

Keywords:

Fonolojia, Athari, Nailotiki, Kiswahili

Abstract

Lugha ya Kiswahili ina mfumo wa kifonolojia ambao una upekee unapolinganishwa na lugha nyinginezo. Tunapochunguza mfumo huu na kuulinganisha na ule wa lugha za Kinailotiki kunadhihirika tofauti anuwai. Makala haya yanalenga kuchanganua namna tofauti kati ya mifumo ya kifonolojia husika inavyochangia makosa ya kimatumizi wakati wazawa wa Kinailotiki wanapoandika kwa Kiswahili. Data ya makala haya inatokana na uchanganuzi wa mawasiliano andishi ya wanafunzi wa shule za upili katika shule teule wilayani Nakuru, Kenya. Wanafunzi husika waliandika insha moja ambayo ilichanganiliwa ili kuibuka na data hii. Makosa yanayotokana na athari za kifonolojia yamechanganuliwa huku njia sahihi ya kuyaandika maneno husika ikionyeshwa. Uchanganuzi huo uliongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Makosa (Corder, 1967). Matokeo ya uchunguzi huu yatawasaidia wanafunzi wa taaluma ya Kiswahili katika kuzua mikakati ya kupunguza makosa ya aina hiyo katika maandishi yao. Aidha, walimu watanufaika na matokeo ya utafiti huu katika harakati za kuwaelekeza wanafunzi kuhusu matumizi sahihi ya Kiswahili hasa kimaandishi. Kuhusiana na taaluma ya Kiswahili kwa jumla, matokeo ya utafiti huu yatachangia kuweka wazi masuala muhimu ya kuchunguzwa katika uwanda wa uchanganuzi makosa.

Downloads

Published

30-04-2019

Issue

Section

Articles