Umilisi Kimsingi wa Mashairi na Namna Unavyoathiri Ufasiri na Uelewekaji wa Ushairi katika Shule za Upili

Authors

  • Gakuo Joseph Kariuki Chuo Kikuu cha Kenyatta Author

Keywords:

Mashairi, Umilisi, Athari, Shule za Upili, Ufasiri

Abstract

Makala haya yanachunguza changamoto za ufasiri na uelewekaji wa mashairi miongoni mwa wanafunzi wa  Kiswahili  wa sekondari nchini Kenya. Tunahoji kwamba ukosefu wa umilisi kimsingi  kuhusu taaluma ya ushairi ni sababu  kuu inayopelekea  wanafunzi wengi kutomakinika katika somo la mashairi. Tunaegemeza tathmini yetu katika mihimili ya nadharia mseto hususan; ya Uhementiki na ya Uhistoria Mpya.  Nadharia ya Uhementiki inadai kwamba ili kuelewa matini nzima, sharti sehemu zote za matini husika zieleweke. Kadhalika, ili kufasiri kila sehemu ya matini kwa ufasaha,sharti mfasiri azingatie matini nzima. Nadharia ya Uhistoria Mpya hutoa msingi maridhawa wa uchambuzi wa matini katika miktadha ya kihistoria. Inaelekeza kuwa; mwingiliano matini uliopo unapatikana kwa kuitazama jamii, mazingira,  historia na utamaduni wa jamii husika na wala, si lazima mhakiki au mfasiri ajifunge kwenye kipengee fulani maalum pekee cha kazi hiyo kama vile lugha. Ni matumaini yetu kuwa makala haya yatatoa kurunzi kwa washika dau kukabiliana na uto-umilisi katika taaluma ya ushairi jambo ambalo tunaamini fika kuwa litasaidia kuondoa kiwi la kutoeleweka kwa ushairi miongoni mwa wanafunzi hao katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Downloads

Published

01-09-2020

Issue

Section

Articles