Utendakazi wa Hadithi za Watoto za Kiswahili katika Kubuni na Kupalilia Muonoulimwengu Wao
Keywords:
Mtazamo Ulimwengu, Sosholojia ya KifasihiAbstract
Makala haya nalenga kubainisha jinsi wahusika katika Hadithi za Watoto wanavyosawiriwa na waandishi tofauti. Hadithi za Watoto za Kiswahili zimeandikwa kwa wingi katika miaka ya hivi karibuni. Ni wazi kuwa mashirika mengi ya uchapishaji yameanza kukazia aina hii ya uandishi. Hii ni kutokana na imani kuwa hadithi hizi zina nafasi muhimu sana katika kuwasaidia wasomaji kufahamu mazingira yao na kujifahamu wao wenyewe. Hadithi za watoto pia zinaweza kuwasaidia katika kukuza uwezo wao wa kuelewa lugha na ulimwengu wao. Ni muhimu pia kutambua kuwa watoto hubuni ulimwengu wao kutokana na yale wanayosoma. Kutokana na msisimko huu wa kukazia aina hii ya uandishi baadhi ya vitabu vya Hadithi za Watoto vilivyoandikwa vimedhirisha mwegemeo usiofaa katika usawiri wa watoto wa jinsia tofauti bila kuwazia athari ya mtindo huo wa uandishi. Kwa hiyo, makala haya yanatathmini namna wahusika wa jinsia mbali mbali walivyokuzwa na baadhi ya waandishi na athari za uteuzi wao. Ni bayana kwamba waandishi wengi wamewasawiri wahusika wa jinsia tofauti kwa usawa lakini ni kweli pia baadhi ya waandishi wamewasawiri wahusika wavulana kwa njia hasi na wasichana kwa njia chanya na kinyume chake pia. Vilevile majukumu yao yametofautishwa kwa njia ambayo hailandani na ukweli wa mambo katika ulimwengu wa sasa. Mjadala wa makala haya utajikita katika vitabu tofauti vya hadithi za watoto.
References
Eagleton, T. (1996). Literary Theory. London: Blackwell Publishing.
Escarpit, R. (1966). Sociology of Literature. London: Frank and Cass.
Glicksberg, C. L. (1987). Literature and Society: The Sociology of Literature. (Wh.). Dandson P. Cambrige: Chadwik Harley.
Grenby, M. O. (2008). Children’s Literature. Edinburg: Edinburg University Press.
Hunt, P. (Mh.). (1994). An Introduction to Children Literature. New York: Oxford University Press.
Jacob, K. (2018). Gender Issues in Young Adults Literature. Indiana: Indiana University Press.
Kabaji, E. (2013). Mwanasayansi. Nairobi: Oxford University Press.
Kimutai, R. (2003). Ndoto ya Riziki. Nairobi: Oxford University Press.
Laurenson, D. T. na Swingewood, A. (1972). The Sociology of Literature. London: Macgibbon Ltd.
Manji, A. (2013). Ndoto ya Mwanafunzi. Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation.
Matundura, B. (2005). Mwepesi wa Kusahau. Nairobi: Phoenix.
Matundura, B. (2007). Taswira Dumifu za Uana katika Fasihi ya Kiswahili ya Watoto. Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi
Matundura, B. (2014). Likizo ya Mkosi. Nairobi: Kenya Literature Bureau.
Mbatiah, A. M. (1999). The Origin and Development of Swahili Thesis Novel in Tanzania. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu cha Nairobi.
Mbuthia, E. M. (2005). A Thematic and Stylistic Analysis of Kiswahili Short Stories. Tasnifu ya Uzamifu chuo kikuu cha Nairobi
Mpesha, N. (2007). Sungura na Binti Mfalme. Nairobi: Phoenix Publishers.
Musembi, N. (2009). Nipe Sababu. Nairobi: Oxford University Press.
Nandwa, R. (2015). Ngamia Mpole. Nairobi: Phoenix Publishers.
Nebbia, C. C. (2016). Gender Stereotypes in Children’s Literature. MA Thesis, University of Northern Iowa.
Ngugi, P. M. (2009). The State of Children Literature in Kenya. Tasnifu ya Uzamifu, Chuo Kikuu Cha Vienna, Austria.
Ngugi, P. M. (2014). Miaka Hamsini ya Fasihi ya Watoto Katika Kiswahili Nchini Kenya. Katika Simala, I. et al. (wh) Twaweza Communications, Nairobi
Njogu, K. na Chimerah, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Odaga, A. B. (1985). Literature for Children and Young People in Kenya. Nairobi: Kenya Literature Bureau
Thiong’o, N. (1978). Literature in Society. In Gachukia, E. na Akivaga, S. K. (Wh.), Teaching of African Literature in Schools. KLB.
Wafula, R. M. na Njogu, K. (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Wamitila K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Books.
Warren, A. na Wellek, R. (1973). Theory of Literature. London: Penguin Books.