Mchango wa Uhakiki-Maeneo katika Ufasiri wa Ploti katika Hadithi Fupi ya Kiswahili
Keywords:
Uhakiki-Maeneo, Mwanda, Homotopiki, Heterotopiki, TrantoAbstract
Utafiti wetu umejikita katika kuhusisha ufasiri wa ploti katika hadithi fupi ya Kiswahili na maeneo ya kijiografia kama yalivyosawiriwa katika hadithi fupi zenyewe. Nadharia mwafaka inayoshughulikia maeneo ya kijiografia katika kazi za kibunilizi ni uhakiki-maeneo. Kupitia usampuli maksudi tuliteua hadithi ya “Ahadi ya Mwana” ya Aidah Mutenyo kutoka diwani ya Safari ya Matarajio na hadithi Nyingine. Matokeo ya uchunguzi wetu yamedhibitisha kuwa uhakiki-maeneo wa maeneo ya kijiografia katika hadithi fupi ya Kiswahili, una manufaa makubwa kwa msomaji wa hadithi fupi ya Kiswahili kwa kuwa ubanifu wa maelezo kuhusu maeneo yenyewe huenda ukasababisha hadithi fupi kutofasirika kwa wepesi na haraka.