Ujasiriamali wa Kiswahili Nchini Kenya

Authors

  • Naomi Jescah Cherono Chuo Kikuu cha Moi Author
  • Nathan Oyori Ogechi Chuo Kikuu cha Moi Author

Keywords:

Ujasiriamali, Viswahili, Kiswahili, Kenya

Abstract

Makala haya yanatathmini shughuli za kiujasiriamali nchini Kenya kwa kutumia ‘Kiswahili’. Shughuli zinazoangaziwa zinajikita katika maeneo mbalimbali ambamo aina fulani za Kiswahili zinajitokeza kwa kuzingatia kwamba kuna “viswahili” vingi vinavyotumiwa nchini Kenya. Neno viswahili katika muktadha huu linatumika kwa maana ya aina mbalimbali za Kiswahili zisizo sanifu ambazo zinapatikana katika shughuli za kila siku zinazoendeshwa na binadamu. Viswahili hivi hutokana na wazungumzaji kutoka makabila na maeneo mbalimbali nchini Kenya wanaokitumia Kiswahili. Tumeendesha mjadala unaojaribu kuonesha jinsi gani ujasiriamali wa Kiswahili umechangia katika kukua kwa Kiswahili katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita. Mjadala huu umeongozwa na dhana ya ujasiriamali kama inavyofasiriwa na taaluma ya uchumi kwa kuiegemeza katika muktadha wa uchumi na lugha. Kwa hivyo, tumeangazia ujasiriamali katika shughuli mbalimbali kama vile vyombo vya habari, biashara kupitia mabango na uchapishaji. Isitoshe, tathmini imefanywa ili kudhihirisha athari chanya na hasi kisarufi na kimawasiliano katika kukua kwa Kiswahili kutokana na matumizi yake kiujasiriamali ili kufichua msambao wa athari hizo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles