Usawiri wa Mhusika Ngoromiko katika Ngano na Masimulizi ya Kijamii
Mifano kutoka Vijiji vya Kware na Kwasadala
Keywords:
Usawiri, Wahusika, Ngoromiko, Masimulizi ya Kijamii, NganoAbstract
Makala hii inachunguza usawiri wa mhusika Ngoromiko katika Ngano za Kichaga. Kwa jumla, mhusika Ngoromiko ni mhusika wa kufikirika anayepatikana katika ngano na masimulizi ya kijamii katika vijiji vya Kware na Kwasadala vilivyopo wilaya ya Hai-Kilimanjaro. Utafiti uliofanywa uliongozwa na malengo mawili ambayo ni kubainisha usawiri wa mhusika Ngoromiko kupitia ngano na masimulizi ya kijamii kutoka vijiji teule na, pili, kubainisha dhamira zinazowasilishwa na mhusika Ngoromiko. Mbinu ya mahojiano na ushuhudiaji ilitumika katika ukusanyaji wa data. Watafitiwa ishirini walihusika katika utafiti huu. Nadharia ya Uhalisiajabu ilitumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data. Kwa jumla, matokeo ya utafiti yanaonesha mhusika Ngoromiko amesawiriwa katika namna ya kutisha na kuogopesha na kuwa ana jicho moja, mguu mmoja na kuwa na makazi katika maeneo yenye kutisha. Vilevile, mhusika huyu amehusishwa na dhamira mbalimbali kama vile chuki, vitisho, vimbwanga vya usiku, ufantasia na kupinga usasa na kuumbatia ukale.