Jazanda na Utambulisho wa Kijamii katika Tawasifu
Mfano wa Riwaya za 'Unbowed, A Memoir' (Wangari Maathai) na 'Nasikia Sauti ya Mama' (Ken Walibora)
Keywords:
Jazanda, Utambulisho, Tawasifu, JamiiAbstract
Riwaya ya tawasifu ni kitengo kisicho na maandishi mengi ya Kiswahili nchini Kenya kama ilivyo tawasifu katika lugha ya Kiingereza. Upekee wa tawasifu ni masimulizi ya mwandishi mwenyewe kujihusu kimaisha kwa lengo la kuuleza ukweli wake binafsi kisanii. Aghalabu, mtunzi wa tawasifu huteuwa yale anayotaka kutambulishwa nayo au kujulikana kwayo kati ya matukio na tajiriba zake nyingi za maisha. Hivyo basi, masimulizi mengi kwenye tawasifu humwelekeza msomaji kumtambua mwandishi kindakindaki kupitia kwa usemi wake mwandishi mwenyewe. Tabia, hulka, imani, matamanio na mazoea huungana kuijenga falsafa ya mwandishi wa tawasifu, ambayo huwa kichocheo kikubwa kwenye uandishi wake; yaani kujitambulisha binafsi na jamii yake. Ni muhimu kwa mtunzi wa tawasifu kuteuwa matukio, wahusika, mbinu na maudhui yanayomjenga yeye na kuitambulisha jamii yake kitabia, kitamaduni na kifalsafa. Mojawapo ya mbinu za kisanii zinazotumika kujieleza kifalsafa ni jazanda. Makala haya yanajadili matumizi ya jazanda kama kipengele cha utambulisho wa kijamii kwenye riwaya za kitawasifu kwa mintaarafu ya nadharia ya semiotiki.