Wahusika wa Kiuhalisiamazingaombwe na Usawiri wa Mivurugo ya Kijamii katika 'Babu Alipofufuka' (2001), 'Dunia Yao' (2006) na 'Bina-Adamu!' (2002)

Authors

  • Sylvester Kimugung Chuo Kikuu cha cha Moi Author
  • Magdaline Wafula Chuo Kikuu cha cha Moi Author
  • Peter Simatei Chuo Kikuu cha cha Moi Author

Keywords:

Wahusika, Uhalisiamazingaombwe, Uswawiri, Jamii

Abstract

Makala haya yanahakiki wahusika wa kiuhalisiamazingaombwe na namna wanavyowasilisha mivurugo ya jamii katika riwaya za Babu Alipofufuka (2001) na Dunia Yao (2006) za Said Ahmed Mohamed, na Bina-Adamu! (2001) ya Kyallo Wamitila. Makala yalibaini kuwa wahusika wa kiuhalisiamazingaombwe wanatumia njia zisizo za kisayansi wala urazini kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwasiliana baina yao. Aidha, wahusika wana nguvu za kimazingaombwe zinazowafanya kufanya kazi mbalimbali kwa urahisi. Kwa ujumla, wahusika wana sifa za kimazingaombwe zinazokaidi kaida za Aristotle na Plato. Makala haya ni muhimu kkatika kuelewa matumizi ya mitindo ya uhalisiamazingaombwe na namna inavyowasilisha mivurugo ya jamii.

Downloads

Published

30-04-2021

Issue

Section

Articles