Uhusiano wa Sera ya Kielimu na Maendeleo ya Kiswahili Nchini Uganda kwa Kuegemea Nadharia ya Uchaguzi na Utekelezaji wa Lugha

Authors

  • Masereka Levi Kahaika Chuo Kikuu cha Makerere Author

Keywords:

Sera, Kiswahili, Elimu, Lugha, Uganda

Abstract

Uganda ni nchi mojawapo iliyomo katika jumuiya ya Afrika Mashariki ambako Kiswahili ni lugha ya mawasiliano kutokana na kifungo 137 cha katiba ya jumuiya. Nchini Uganda kumekuwepo maandiko mengi kuhusiana na matumizi ya Kiswahili katika taasisi za kielimu ikiwa ni pamoja na ripoti ya Kajubi ya 1987, Government White Paper on Education ya 1992 pamoja na CURASSE [1] ya 2013 iliyopendekeza Kiswahili kuwa lugha ya lazima katika shule za msingi na za upili nchini kote. Pamoja na mapendekezo hayo yote, vyuo vyote vya taifa pamoja na vya kibnafsi vilichukua jukumu la kufundisha walimu ambao wamehitimu katika kufundisha Kiswahili katika viwango vyote vya kielimu. Pamoja na kuweko kwa walimu ambao wamehitimu kupitia vyuo hivyo, serikali haijatekeleza suala la kufanya Kiswahili kuwa somo la lazima katika shule za msing na upili. Kwa kuongozwa na nadharia ya uchaguzi na utekelezaji wa lugha pamoja na nadharia ya upangaji lugha, makala haya yanabainisha uhusiano wa sera ya kielimu na maendeleo ya Kiswahili ilivyo nchini Uganda na kupendekeza njia za kuinua hali hiyo. Data ilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa matini zilizoandikwa kuhusu Kiswahili.

 

[1] CURASSE: Ni kifupisho cha Curiculum Reform Assesment and Evaluation.

Downloads

Published

30-04-2018

Issue

Section

Articles