Changamoto Zinazokumba Uchanganuzi, Ufasiri na Ufunzaji Ushairi wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya
Keywords:
Ushairi, Ufasiri, Shule za Upili, KenyaAbstract
Makala haya yanaangazia baadhi ya changamoto zinazokumba taaluma ya ufasiri, uelewekaji na ufundishaji wa somo la ushairi katika shule za sekondari nchini Kenya. Mawazo na kauli zinazoshereheshewa katika makala haya zinazotokana na utafiti wa kisayansi uliofanyika katika kaunti mbili za Mombasa na Trans Nzoia. Pamoja na kufafanua changamoto husika, nimejizatiti vilevile kutoa mapendekezo na suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo. Tunataraji kuwa utafiti huu utanufaisha na kuimarisha ufunzaji wa ushairi na lugha ya Kiswahili kwa jumla.