Ujifunzaji wa Kiswahili Miongoni mwa Wakinga

Authors

  • Arnold B. G. Msigwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Author

Keywords:

Usasanyuzi Dosari, Dosari, Makosa na Uamiliaji Lugha

Abstract

Lengo la makala haya ni kueleza dosari zinazofanywa na wajifunzaji wa lugha ya pili (kuanzia sasa Lg2) katika Jamii ya Wakinga. Usasanyuzi dosari ni eneo muhimu katika taaluma ya Isimu Tumizi na katika taaluma ya ujifunzaji wa Lg2. Umuhimu wake unatokana na ukweli kwamba, wajifunzaji wengi wanaojifunza Lg2 hufanya dosari mbalimbali katika hatua ya kujifunza lugha hiyo. Vilevile, ni mbinu pangilifu ya kuchanganua dosari za mjifunzaji lugha. Kitaaluma dosari si kitu kibaya bali ni kipengele muhimu katika mchakato wa ujifunzaji lugha. Dosari husaidia kutambua mchakato changamani wa maendeleo ya lugha Na namna pangilifu ya kubaini, kueleza na kufafanua dosari za mjifunzaji lugha. Pia, dosari zinaweza kusaidia kutoa uelewa wa mchakato wa kuamili Lg2. Makala haya kwa hiyo yanalenga kuchunguza kwa nini wajifunzaji wa lugha ya Kiswahili katika jamii Wakinga hushindwa kumudu vema lugha ya Kiswahili licha ya kuwa ni somo la lazima tangu shule za msingi hadi sekondari za juu. Makala yanahitimisha kwamba dosari hizi kwa kiasi kikubwa zinachangiwa na athari za lugha yao ya kwanza na umbali wa kijiografia kutoka kitovuni mwa lugha ya Kiswahili.

Downloads

Published

30-06-2019

Issue

Section

Articles